Takriban watu 73 wamedaiwa kufariki kufuatia mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari wakati wa pilka pilka nyingi katika mji mkuu wa Mogadishu nchini Somalia.
Mlipuko huo ulitokea katika kituo kimoja cha kukagua magari katika eneo la makutano ya barabara mjini Mogadishu. '
'Mlipuko huo ulikuwa mbaya mno na naweza kuthibitisha kwamba zaidi ya raia 20 waliuawa , huku wengine wengi wakijeruhiwa'', afisa wa polisi Ibrahim Mohamed alinukuliwa na kituo cha habari cha AFP akisema.
Dkt Mohamed Yusuf, mkurugenzi wa hospitali ya Madina aliambia kitengo cha habari cha AP kwamba wamepokea miili 73 . Idadi ya watu waliofariki inatarajiwa kuongezeka
Hakuna kundi ambalo limekiri kutekekelza kitendo hicho lakiini wapiganaji wa kundi la al-Shabab wamekuwa wakitekeleza mashambulizi ya mara kwa mara katika taifa hilo.
Al-Shabab - kundi la wapiganaji linaloshirikiana na kundi la kigaidi la Al-Qaeda limekuwa likitekeleza mashambulizi kwa zaidi ya miaka 10, lilifurushwa kutoka mji mkuu wa Mogadishu 2011 lakini linadhibiti maeneo ya taifa hilo.

No comments :
Post a Comment