Above: The Dar Es salaam Regional Commissioner Mr Paul Christian Makonda who has been banned by the Trump administration from entering the United States of America for gross violations of human rights - according to the US .
JE NI SAHIHI MSANDO KUJIBU MASUALA YA DIPLOMASIA?
Na Thadei Ole Mushi.
Nimeisoma Barua ya Msando yote aliyowaandikia USA.
1. Achana na Makosa ya Address aliyoyafanya Brother Msando twende kwenye Hoja nyingine za barua ya Msando. Kwenye barua ile kuanzia mwanzo Hadi Mwisho Msando kaonyesha kuwa hata Marekani huwa wanavunja haki za binadamu. Msando anataka kutuaminisha kuwa Marekani leo wakiamua Kula Kinyesi na sisi ni sawa kula kinyesi pia. Hakuna mahali ambapo Msando kaweza kusema Kama ni kweli haki za Binadamu zinavunjwa ama lah!... Kwa kifupi Msando anatuambia kuwa ni Kweli tumekiuka haki za Binadamu simply kwa kuwa Marekani nao wanazivunja.
2. Issue za Kidiplomasia hujibiwa Kidiplomasia na hupitia Chanel ambazo ni sahihi. Kilichofanywa na Msando ni kutaka kufurahisha watawala lakini akumbuke kuwa barua yake inazidi kuzorotesha uhusiano wetu na Marekani. Mh Kabudi sio mjinga kutafakari, Serikali kwa ujumla sio wajinga kutokumjibu Pompeo, wanatafakari kwa namna gani wanaweza kusulihisha mgogoro huu wa Kidiplomasia. Fani hii ya Diplomasia watu huisomea huwezi kukurupuka tu from no where mtu individual ambaye Hana taaluma hiyo kuanza kutuhumu mataifa Mengine. Kwa bahati mbaya kabisa barua ile copy yake ameielekeza kwa Rais wetu. Msando Hana tofauti na vijana waliovamia ubalozi wa S.A kudai Bombadia.
3. Msando naye kaingia kwenye Makosa yale yale kuwa naye anatetea ukiukwaji wa haki za Binadamu. Kwa maana hiyo Msando Siku akiwa Kiongozi hawezi kutuwakilisha Tena Marekani pamoja na washirika wake.
4. Serikali na hasa Rais hahitaji utetezi Sana anachohitaji ni Solutions, tunatetea Sana badala ya kutoa solutions. Barua ya Msando haitoweza kuitisha Marekani na Wala Marekani haitobadili msimamo kwa sababu ya barua ya Msando. Kwa maana hiyo bado tatizo linabaki pale pale na linaweza kukuzwa kwa barua hii ya Msando. Tumepoteza uwezo wa kutoa Solutions kwa sababu ya kusaka madaraka na Vyeo.
5. Kuna kasumba imeibuka kuwa ili uwe mzalendo Kila Jambo la Serikali ni la kutetea, nchi hii haiwezi kujengwa kwa kutetea makosa, nchi hii itajengwa kwa kuyaondoa makosa, kuambiana ukweli kuwa hili hapana lile sawa.
Wahenga walisema "two wrongs don't make a right". Narudi Jalalani..
Ole Mushi
0712702602
Kaka Albert, wife anamimba pevu unamtia kwenye ndege ili mtoto apate uraia wa Marekani lakini hujali hali ya wife. HALAFU UNASEMA YOU HAVE NO SOFT AFFILIATION WITH USA, KWANINI UKAHATARISHA MAISHA YA WIFE WAKO PAMOJA NA MTOTO WAKO TUMBONI? Hujui kama mwanamke akiwa na mimba zaidi ya miezi 4 harusiwi kupanda ndege? What you did was not an abuse on your own wife? Wacha blah blah hizo. Sote tunajua kuwa umetumwa ili uandike barua hii. Imehusu nini kumpelekea copy Rais, Makamu wa Rais, Makonda na watu tele? Wewe ungeliitoa kwenye media tu. Hii inaonesha wazi kuwa umetumwa na sio kazi yako. Msitufanye Watanzania kuwa ni wajinga na mbumbumbu hivyo.
ReplyDeletewe provide Loans with 3%.Business Loans, Home Loans, Mortgage Loans,Personal Loans, Car finance,real estate Loans,Construction loans,Investments Loans, Email: capitallendinghelpdesk@gmail.com
ReplyDelete