Uingereza imeainisha misimamo mikali kwa ajili ya ufunguzi wa majadiliano ya baadaye na Umoja wa Ulaya hii leo na kusema itaratibu agenda zake yenyewe badala ya kuzingatia sheria za Umoja huo kuhakikisha utekelezaji wa biashara usiokuwa na vipingamizi.
Baada ya kujiondoa rasmi katika Umoja wa Ulaya siku ya Ijumaa, Uingereza sasa lazima iingie katika mazungumzo kuhusu uhusiano wa baadaye wa kibiashara na Umoja huo, ambapo matokeo yake yataanza kutekelezwa baada ya kipindi cha mpito cha mwaka mmoja kitakachokamilikia mwishoni mwa mwaka huu.
Serikali ya waziri mkuu Boris Johnson imetuma ujumbe wa haraka katika Umoja huo kabla ya mazunguzmo kuanza mwezi Machi kwamba kulingana na Johnson, Brexit inamaanisha Uhuru ni mkuu kushinda uchumi.
Mara kwa mara, Umoja huo umeiambia Uingereza kuwa kiwango cha kufikia soko lake kitategemea jinsi Uingereza itakavyokubali kuzingatia ''kiwango cha usawa,'' hii ikimaanisha sheria za viwango vya mazingira, sheria za soko la kazi na usaidizi wa serikali.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment