dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, February 19, 2020

CHADEMA yatoa tamko kuhusu Dkt. Mashinji kuamia CCM!

Baada ya aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA Dk Vicent Mashinji kuamia CCM Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini Tanzania (Chadema) kimesema walishaona dalili na ndiomana awakumchagua tena.

Mkurugenzi wa Itikadi, Uenezi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema, “Dk Mashinji tulimjua kuwa alikuwa amepanga safu ya mgombea wake wa uenyekiti (wa Chadema) ambaye ni Mwambe (Cecil-alirejea CCM juzi akitokea Chadema).”

“Mgombea wake wa urais ambaye ni Sumaye (Frederick- waziri mkuu wa zamani) naye amerudi CCM, sekretariati aliyokuwa ameiandaa nayo itaondoka Chadema ni suala la muda tu.”
"Dr mashinji amevunja record ya kukaa kwenye chama kwa muda mfupi kuliko katibu yoyote yule tulimshitukia angetuunza amekaa takribani miaka mitatu ni katibu mkuu ambaye amevunja rekodi kwa kukaa muda mfupi madarakani atuwezi kusema ni pengo kama ingekuwa ni pengo ingekuwa ni kwa Dkt. Slaa ambaye alikaa muda mrefu zaidi kuliko wote". alisema Mrema.

Dk Mashinji amejiunga CCM leo katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam ikiwa imepita miezi miwili tangu ufanyike mkutano mkuu wa Chadema na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kutompendekeza tena kuwa katibu mkuu.

Badala yake, Mbowe alimpendekeza mbunge wa Kibamba, John Mnyika kuwa katibu mkuu wa tano wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

No comments :

Post a Comment