Nyama nyeupe ni ipi?
hii ni nyama ambayo ikichinjwa inakua na rangi nyeupe kabla ya kupikwa mfano halisi ni nyama ya kuku, bata, mbuni, ndege wote na samaki aina zote.nyama nyekundu ni ipi?
hii ni nyama ambayo ikichinjwa inakua na rangi nyeupe kabla ya kupikwa, mfano ni nyama za wanyama wote kama nguruwe, mbuzi, ng'ombe, na kadhalika.
kumekua na mijadala na maswali mengi kutaka kujua faida hasa za nyama hii nyeupe ukilinganisha na ile nyekundu naleo ntazitaja faida hizo kwa kifupi..
- upatikanaji wa virutubisho muhimu vya siku kwani nyama nyeupe ina mafuta kidogo, vitamin, protini na nguvu kwa ajili ya shughuli za kila siku.
- nyama hizi zina amino acid nyingi ambayo ni muhimu kwa ujenzi wa seli za binadamu na ukuaji wa nywele kwa ujumla.
- nyama hizi zina mafuta kidogo sana ambayo sio hatari kwa afya ya moyo na mfumo mzima wa mwili wa binadamu.
- nyama samaki ina kemikali inayoitwa omega 3 ambayo haitengenezwi na miili yetu lakini ni muhimu sana kwa kupunguza kiasi cha lehemu au cholestrol mwilini.
- nyama ya kuku ina kiasi kikubwa cha selemium ambayo ina kazi ya kuzuia saratani mbalimbali kwenye miiili yetu.
- nyama nyeupe ni nzuri sana kama ikitumika kama sehemu ya diet kwa ajili ya kupunguza uzito kwani ni laini na mwili unaimeng'enya kirahisi sana.
- samaki ina vimelea ambavyo ni muhimu sana kwa ajli ya kuzuia tatizo la kusahau sana uzeeni ambalo tafiti zimeonyesha kwamba nyama nyekundu huchangia kwa tatizo hili,
- kiasi cha phosphorus kipatikanacho kwenye samaki ni muhimu sana kwa ajili ya kusaidia macho yaendelee kuona vizuri.
- nyama nyeupe inaweka kiwango cha sukari mwilini katika hali nzuri sana na inaweza kuwafaa sana wagonjwa wa kisukari.
- nyama hii haikai sana tumboni ukilinganisha na ile ya mayai hivyo huweza kuzuia tatizo la saratani ya utumbo ambalo ni kubwa sana kwa watumiaji wa nyama nyekundu.
/Muungwana.
No comments :
Post a Comment