Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, February 2, 2020

MHE. ZITTO KABWE NA MHE. NASSOR MAZRUI WATINGA JIJINI TORONTO!


Pichani: Mhe Zitto Kabwe (5 kutoka  kulia) na Mhe Nassor Mazrui (3 kutoka kulia) wakipiga picha ya pamoja na weneji wao baada ya kuwasili Pearson International Airport, Toronto. Wapili kutoka kulia is our flamboyant 'Uncle'.
Jiji la Toronto lamkaribisha Mhe Zitto na Mhe Mazrui.
Zitto Kabwe, kiongozi wa Chama Cha ACT-Wazalendo ameandika kwenye tweeter yake kuwa yeye na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Mhe. Nassor Mazrui wamefika salama jijini Toronto, Canada.

Zitto akiendelea kwenye tweeter yake ameandika kuwa..."Tunaendelea na ziara yetu ya kimataifa, kuonana na Watanzania wanaoishi nje (Diaspora) na kuzungumza na serikali za nchi hizo na Taasisi za Kimataifa ili kuhakikisha kuwa Uchaguzi wa Tanzania unakuwa Huru, wa Haki na unaoaminika (credible".

Zitto na Mazrui leo Jumaapili watawahutubia Wana-Diaspora kutoka Tanzania wanaoishi Toronto na katika vitongoji vyake, ili kupata maoni yao kuhusu masuala ya Watanzania wanaoishi nje kwaajili ya ilani ya Chama cha ACT Wazalendo kwa Uchaguzi Mkuu unaokuja.

Maoni makubwa ya Wana-Diaspora inasadikiwa kuwa yatakuwa juu ya suala la uraia pacha na inategemewa mkutanoni Mhe Zitto ataulizwa ili atamke kinagaubaga juu ya msimamo wa Chama chake kuhusu suala hilo.


Kama inavyojulikanwa kuwa serikali ya awamu ya tano haina mpango wa kuikubali sera ya uraia pacha kwa Tanzania, japokuwa nchi zote jirani na Tanzania zina sera hio. Zanzibar kwa upande wake ilitaka kuleta kitu kinachokaribiana na uraia pacha, lakini inaonesha juhudi zake either zimegonga mwamba au zinaendelea kidogo kidogo sana.

Suala la uraia pacha ni jambo muhimu sana kwa Wana-Diaspora, kwasababu wengi wao wanataka kuekeza nyumbani, lakini hawapendelei kuenda kuwekeza kama wageni kwavile wao wamezaliwa Tanzania.

Kama Mhe Zitto Kabwe atawahakikishia Wana-Diaspora leo mkutanoni kuwa serikali yake itaukubali uraia pacha, basi atawasomba Wana-Diaspora wengi kuelekea upande wa Act Wazalendo katika uchaguzi ujao.

Mkutano  wa Mhe. Zitto na Mhe. Mazrui utakuwa leo Jumapili saa 9 mchana, katika Hall la SACKVILLE STREET, DOWNTOWN TORONTO, ONTARIO, M5A 3G1 - kama inavyonakiliwa katika fliers zinazosambazwa. 


Kama utafika mkutanoni basi wahi mapema kwasababu Hall linategemewa sio kujaa bali kufurika, kwani wengi wanataka kumuona Mhe Zitto hasa baada ya kupewa umaarufu zaidi wa ghafla na Bunge la Tanzania na kuwa the talk of the whole country and in the Diaspora, kutokana na msimamo wake wa kuwatetea wasichana wanaopata mimba za bahati mbaya wakati wapo masomoni!

No comments :

Post a Comment