Tanzania now catches up with Kenya in infrastructure projects
Kwa muda wa zaidi ya miaka 35, Kenya imekuwa ikiongoza kwa afrika mashariki katika m maendeleo na uandikishaji wa miradi mipya .Ni katika miaka ya 2016-2017 Ethiopia ikaingia katika kusuguana na kenya katika gharama za miradi iliyoandikishwa na serikali zao.
Lakini kwa mara ya kwanza kutoka katika ripoti ya kampuni ya kimataifa deloitte imeonyesha kwa mwaka 2019,Tanzania ama walikuwa wakiita the sleeping giant imepindua meza kwa kuweza kusajili miradi mikubwa 51 yenye gharama ya 61.3 billion usd sawa na Tzs Trilioni 150.hii ni sawa na asilimia 41% ya miradi inayoendelea katika nchi za afrika mashariki.
Nchi ya kenya imekuwa ya pili kwa kusajili miradi 51 yenye jumla ya thamani ya dola billioni 30 billion usd ama tzs Trilioni sabini sawa na asilimia 24% ya miradi inayoendelea afrika mashariki.
Tanzania imekuwa na miradi inayoendelea kama standard gauge, bwawa la umeme, mchuchuma ama lng plant, ilhali kenya imeendelea katika miradi ya std gauge treni, barabara.
Ripoti hii imezihusisha nchi zilizoko afrika mashariki ambazo ni burundi, djibouti, Eritrea, Ethiopia, kenya, Rwanda, shelisheli, Somalia, Tanzania na Uganda.
/Jamii Forums
No comments :
Post a Comment