Budget hii ni ya kuiwezesha Jumuiya hii kufanya kazi zake katika mwaka 2020.
BoT iliahidi mkutanoni kuwa katika Ramadhani ya mwaka huu wa 2020 itaendelea na kawaida yake ya kufutarisha katika kisiwa cha Unguja na Pemba.
Pia, itaendelea kugawa tende kwa waumini wa kiislamu wa misikiti mbali mbali pamoja na Madrasa za akina mama na kuwapatia eid watoto wanaowadhamini Pemba na Unguja.
Katika mkutano wa Board wa leo, Zacadia imepanga kupeleka tena Zanzibar mabuku ya kusomea pamoja na vitu kama vile vitanda vya hospitali na wheelchairs.
Ikumbukwe kuwa miaka miwili nyuma (2018), Zacadia ilipeleka Zanzibar Container zima la futi 40 ambalo lilijazwa vitabu vya kila aina vyenye thamani zaidi ya shilingi bilioni mbili na nusu, pamoja na zana tafauti kwaajili ya matumizi ya hospitalini. Vitabu hivyo vilivyopelekwa Zanzibar vilikuwa zaidi ya vitabu 25,000 na vilikuwa katika fani tafauti za taaluma, kama vile Pure Science, Agriculture, Ecology, Medicine, Business, Mathematics, Engineering Science and Social Studies.
Bodi ya Trustees imeweka wazi mkutanoni kuwa jitahada za kupata ID zinaendelea na kuwa sera ya Diaspora inategemewa kupelekwa kwenye Baraza La Wawakilishi katika mwezi wa May, 2020.
Madhumuni ya mkutano huu wa leo wa BoT ulikuwa ni kuweka road map katika shughuli za Jumuiya hii kwa mwaka huu mpya pamoja na kujifunza kutokana na mapungufu ya mwaka uliomalizika.
No comments :
Post a Comment