Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Mpoki Ulisubisya kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam tarehe Jumatatu Mei 20, 2019.
"Yah: Mkutano wa Balozi na WanaDiaspora – Tarehe 9 Februari, 2020.
Tafadhali rejeeni barua pepe ya Ubalozi iliyotumwa kwenu tarehe 21 Januari 2020 kuhusu kuahirishwa kwa mkutano wa Balozi na Wana-Diaspora. Katika barua pepe hiyo, tuliwaomba wana-Diaspora kupitia Viongozi wao wachague siku ambayo itakuwa muafaka kukutana na Mhe. Balozi. Viongozi hao wameufahamisha Ubalozi kuwa wako tayari kukutana na Mheshimiwa Balozi siku ya Jumapili, tarehe 9 Februari, 2020. Kufuatia tarehe hiyo kukubalika, Ubalozi unawataarifu kuwa, Mheshimiwa Balozi anawakaribisha Watanzania wenzake tarehe 9 Februari, 2020 kuanzia 10:00 jioni, Tanzania House, 2191 Niagara Drive, ON K1H 6G5. Kwa kuwa siku inayofuata ni siku ya kazi, mkutano huo utamalizika saa 01:00 jioni ili washiriki wakajipange na majukumu mengine.
Tafadhali taarifa hii ifikishe kwa wengine.
Nyote mnakaribishwa, karibuni sana.
UBALOZI - OTTAWA"
Click here for the previous communication: https://zanzibarnikwetu.blogspot.com/2020/01/ubalozi-wa-tanzania-nchini-canada.html
No comments :
Post a Comment