dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, June 20, 2020

ELECTIONS ZANZIBAR 2020: WASIFU WA PROFESA MAKAME MNYAA MBARAWA!


KWA MAELEZO YA MWANZO GONGA HAPA:
Prof. Makame Mnyaa Mbarawa alizaliwa mwaka 1961 Chokocho Kisiwani Pemba na kupata elimu ya msingi na sekondari katika Skuli ya Chokocho ambayo kwa sasa ni Skuli ya Mkanyageni iliyopo Wilaya ya Mkoani, Pemba na baadae aliendelee na elimu ya ufundi katika Chuo cha Ufundi cha Karume huko Mbweni, Zanzibar na kuhitimu mwaka 1981.

Mwaka 1985 Prof. Mbarawa alipata nafasi ya kusoma nje ya nchi huko Urusi akisomea Uhandisi wa Mitambo ya meli (Marine Engineening) ambapo alijiunga na Chou cha “Astrakhan Technical Institute of Fisheries” sasa kinatambulika kama Astrakhan State Technical University (ASTU) ambapo mwaka 1992 alihitimu shahada ya uzamivu katika fani ya uhandisi Mitambo ya meli. Mwaka 1994 alijiunga na Chuo Kikuu cha New South Wales, Sydney, Australia na kuhitimu shahada ya uzamivu (PhD), mwaka 1999.


Kati ya mwaka 2000 na 2014 Prof. Mbarawa alihudhuria programu za mafunzo mbalimbali kama vile mafunzo ya usimamizi wa miradi huko Chuo Kikuu cha Stellenbosch, Bussiness School, Afrika ya Kusini mwaka 2000; Mafunzo ya stadi katika ustadi wa kufundisha (Competence in teaching skills), Pretoria Tecknikon, Afrika ya Kusini mwaka 2001; Mafunzo ya “Innovation for Economic development”, Harvard Kennedy School, Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani mwaka 2014; Mafunzo ya “Cybersecurity: Intersection of Policy and Technology”, Harvard Kennedy School, Chuo Kikuu nchini Marekani mwaka 2015.
Kati ya mwaka 1981 na 1985 alifanyakazi Idara ya Usafiri Baharini, wakati huo ilikuwa chini ya Wizara ya Mawaswiliano na Uchukuzi, Zanzaibar na Shirika la Meli Zanzibar. Aidha baada ya masomo yake ya uzamili kati mwaka 1993 na 1994 alifanyakazi tena kwenye Shirika la Meli Zanzibar.

Mwaka 1999, Prof. Mbarawa alijiunga na Chuo Kukuu cha Stallenbosch, Afrika ya Kusini kama Mtafiti katika Kituo cha Uhandisi wa Magari. Baadae Prof. Mbarawa alifanyakazi katika Chuo cha Technikon Pretoria kwa sasa kinatambulika kama Chuo kikuu cha Teknolojia cha Tshwane (Tshwane University of Technology), Pretoria, Afrika ya Kusini mwaka 2000 akiwa kama Mhadhiri Mwandamizi katika idara ya Uhandisi Mitambo. Mnamo mwaka 2005 alipandishwa na kuwa Profesa Mshiriki (Associate Professor) na mwaka 2009 alipandishwa na kuwa Profesa Kamili (Full Professor) na Mkuu wa Idara ya Uhandisi Mitambo. Kutokana na taaluma, utafiti na kazi yake ya uhadhiri Prof. Mbarawa amefanya tafiti mbalimbili kwenye maeneo ya “alternative fuels, filtration combustion, soot formation”, n.k. Aidha, amesimamia Wanafunzia mbalimbali wa shahada ya uzamili na uzamivu na ameandidika machapisho ya kitafiti zaidi ya 50. Kati ya Wanafunzi hao wa Uamivu na Uzamili ambao Prof. Mbarawa aliwasimamia sasa hivi wanafanyakazi kwenye Taasisi mbali hapa nchini.

Kwa upande mwengine, mwaka 2010 aliteuliwa na Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Daktari Jakaya Kikwete, kuwa Mbunge na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Katika kipindi hicho alisimamia miradi mbalimmbali ya sekta ya mawasiliano, sayansi na teknolojia kama vile: ujenzi wa mkongo wa Taifa wa mawasiliano (NICTBB), Ujenzi wa kituo mahiri cha kuhifadhia data (Nation Data Cente), Mabadiliko ya mfumo wa utangazaji kutoka analogia na kuhamia mfumo wa kidijitali, Uanzishwaji wa mfumo wa mawasiliano ya simu (TTMS), n.k. Alihudumia Wizara hiyo mpaka mwaka 2015.

Aidha mwaka 2015, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Daktari John Pombe Joseph Magufuli, alimteu Prof. Mbarawa kuwa Mbunge na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Kwenye Wizara hii chini ya Uongozi mahiri wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Prof. Mbarawa alisimamia kwa mafanikio makubwa miradi mbalimbali ya kimkakati kama vile: Ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme (SGR) kutoka Dar es Salam mpaka Dodoma ambao unaendelea kutekelewza kwa sasa, Ufufuaji wa Shirika la ndege la ATCL ambapo ndege 7 mpya zilinunuliwa, Uboreshaji wa Bandari ya Dar es salam, Ujenzi wa gati mpya huko Mtwara ambao unaendelea kutekelewza kwa sasa, Ununuzi na Ufungaji wa Scanners 6 mpya Bandari ya Dar es salam, Ununuzi na Ufungaji wa Rada 4 za kisasa kwenye viwanja vya ndege vinne, Ujenzi wa Jengo la Abiria No. 3 Uwanja wa ndege wa Dar es salaam; Usimamizi wa mnada wa kwanza wa masafa ya 700Mhz nchini, Ujenzi wa mabarabara na madaraja, Uanzishwaji wa Shirika la Reli na Shirika la Wakala wa Meli, n.k. Alihudumia Wizara hiyo mpaka tarehe 30 June mwaka 2018.

Prof. Mbarawa aliteuliwa tena na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Daktari John Pombe Joseph Magufuli, kuwa Waziri wa Maji tarehe 1 July mwaka 2018. Kwenye Wizara hii chini ya Uongiozi mahiri wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Prof Mbarawa amefanya mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutendaji. Kwanza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) imeanzishwa ili kukabidiliana na changamoto kubwa ya usimamizi wa miradi ya maji hasa Vijijini. 


Pili kutokana na changamoto za gharama kubwa ya miradi na kuchelewa kukamilika kwa miradi, utaratibu mpya wa utekelezaji wa miradi ya maji kwa kutumia utaratibu wa force account umeanza kutumika. Tatu, Prof. Mbarawa amesimamia miradi mikubwa ya maji ya kimkakati kwa mafanikio makubwa kama vile mradi wa maji wa jiji la Arusha ambao unagharimu Shilling Bilioni 520 unaendelea kutekelewza kwa sasa, mradi wa maji kutoka ziwa Victoria kupeleka Tabora ambao unagharimu Shillingi Bilioni 622, miradi wa maji wa miji 28 ambao unagharimu Shillingi Trilioni 1.2 unaendelea kutekelewza kwa sasa, n.k. 

Kutokana na maboresha mbalimbali yaliyofanyika takwimu zinaonesha kuwa wastani wa idadi ya watu wanaopata huduma ya maji safi na salama vijijini imeongezeka kutoka asilimia 47 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 70.1 mwezi Machi mwaka 2020. Kwa upande wa mijini, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji imeongezeka kutoka asilimia 74 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 84 mwezi Machi mwaka 2020.

Kwa upande wa harakati za kisiasa Prof. Mbarawa, alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi kutokea 2007 mpaka mwaka 2017 na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi kuanzia mwaka 2012 -2017.

No comments :

Post a Comment