dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, June 16, 2020

Profesa Mbarawa ajaribu kuwaangukia wajumbe wa CCM Zanzibar!


FIRST UPDATE YOUR THOUGHTS BY CLICKING THE LINKS BELOW:


Taarifa toka Unguja zinasema kwamba mmoja ya watangaza nia kugombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM Profesa Makame Mbarawa amewasili kisiwani humo akitafuta kuungwa mkono na makundi mbalimbali.

Inaelezwa kwamba katika orodha ya shughuli alizofika kufanya Unguja ni kumwangukia Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein. Mbarawa hajafika kuzungumza na kiongozi huyo mwenye nguvu CCM Zanzibar kwa zaidi ya miaka minne sasa, na hatua hiyo ya kutaka kumuona katika dakika hizi za lala salama inachukuliwa kuwa ni ya “kuomba msamaha” na kuomba Dkt Shein kumuunga mkono katika nia yake ya kutaka kuteuliwa na CCM kugombea Urais Zanzibar 2020.



Hata hivyo hilo huenda lisifanikiwe kwani Mbarawa amewahi kunukuliwa siku za nyuma akibeza baadhi ya miradi mikubwa yenye tija ya serikali ya awamu ya saba (SMZ) chini ya Dkt. Shein kama meli za uvuvi (Sehewa I &II) na ile ya MV Mapinduzi II.

Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa amezunguka pia na kuonana na baadhi ya wenyeviti wa CCM wa mikoa na baadhi ya viongozi wa chini huku wengine wakigoma kuonana naye mpaka pale kampeni zitakoruhusiwa rasmi na CCM.
“Huyu mtu hakuwahi kuja kuniona, tena kuna wakati Bungeni katuita wapiga kelele tuso maana wakati Bi Saada Mkuya alipojaribu kumkumbusha kupigania maslahi ya Wazanzibari. Nakwambia tu ukweli ndugu yangu mie na wenzangu hatuna la kuzungumza naye kwa sasa,” amenukuliwa mmoja ya viongozi waandamizi wa CCM Zanzibar.

Baadhi ya viongozi hao wameongeza kwamba Profesa Mbarawa amekuwa akiongea kiukali alipokutana nao na kujifanya kama katumwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa jambo ambalo si kweli na kinyume kabisa na falsafa na hulka ya Mwenyekiti wa sasa wa CCM Rais Dkt. Magufuli ambaye haendeshi chama wala serikali kwa mtindo huo anaoonesha Mbarawa.

“Hili lake lishavunda siku nyingi tangu alipojaribu Ubunge. Halina ubani. Kule Pemba hadi kijijini kwao hatakiwi na hapa Unguja hatakiwi kabisa. Sasa kaja na urongo wa kutumwa na Bwana Mkubwa na sisi twafahamu Bwana Mkubwa hafanyi kazi kwa staili hiyo anayojinasibu nayo yeye”, kiliongeza chanzo hicho.

CCM tayari imetangaza ratiba yake ya zoezi la kuchukua na kurejesha fomu ili kuteua Mgombea wa Urais Zanzibar 2020. Chama hicho kimepanga kuteua mgombea wake Julai 10 mwaka huu na kumpitisha siku mbili baadaye. Mgombea atakayepitishwa na CCM ataingia kuchuana na upinzani Oktoba 25. Upinzani mkubwa unatarajiwa kutokea chama cha ACT Wazalendo.


1 comment :

  1. DIASPORA FOR PROFESA MBARAWA!!
    WAZANZIBARI WENGI WALIOKO NJE YA NCHI DIASPORA WANAONA KUWA ZANZIAR ITAKUWA SALAMA KAMA PROFESA MBARAWA ATAKUWA RAISI WA ZANZIBAR, SHIME WANA KAMATI KUU KUMUUNGA MKONO MBARAWA

    ReplyDelete