Saniniu Kuryan Laizer akionyesha mawe ya Tanzanite ya awali yaliyompatia hadhi ya Ubilionea
Mtanzania Saniniu Kuryan Laizer ambaye hivi karibuni aligeuka kuwa bilionea baada ya kupate mawe ya madini ya Tanzanite yenye thamani ya shiling bilioni 7.8, ameagundua jiwe lingine la Tanzanite lenye thamani ya Shilingi milioni 140.Jiwe hilo lina uzito wa kilo 6.33.
Jiwe la sasa alilolipata Saniniu Kuryan Laizer ambaye ni mchimbaji madini mdogo linasemekana kuwa ni jiwe la pili kwa ukubwa kuwahi kupatikana katika machimbo ya madini hayo kaskazini mwa milima ya Mirelani .
Mwezi mmoja tu uliopita alipata madini ambayo moja lilikua na kilo 9.2 likiwa na thamani ya bilioni 4.5 na la pili lina kilo 5.8 lenye thamani ya shilingi bilioni 3.3.
Serikali inatarajiwa kukabidhiwa jiwe la hivi karibuni kutoka kwa Bwana Laizer ambapo inatarajiwa kuwa atakabidhiwa pesa kutokana na jiwe hilo.
Saniniu Kuryan Laizer mwenye umri wa miaka 52, ni mume wa wanawake wanne na amejaliwa watoto 30.
Baada ya kupata madini hayo Bilionea Laizer aliyafikisha katika kituo cha utambuzi. Na serikali ya Tanzania iliyanunua madini hayo kwa thamani ya bilioni saba na milioni mia saba za kitanzania.
Madini hayo yalikabidhiwa kwa serikali na BLazier ambaye ni mkazi wa Simanjiro akapatiwa fedha zake huko Mkoani Arusha kaskazini kwa Tanzania.
Bwana Laizer alisema kuwa anapanga kujenga shule na kujenga kituo cha biashara kwao baada ya kupata pesa alizolipwa kutokana na mawe aliyoyapata awali.
Kupitia mtandao wa Twitter Wizara ya madini ya Tanzania ilimtambua Mtanzania huyo kama bilionea.
Kwa mujibu wa wizara ya madini nchini humo madini ya uzito huo hayajawahi kupatikana katika machimbo ya Tanzanite
Tanzanite ni madini yanayopataka na kuchimbwa nchini Tanzania pekee.
Mauzo ya madini hayo kwa mwaka 2019 duniani yalikua zaidi ya dola milioni 50 za kimarekani.
Yaligunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mnamo mwaka 1967, katika eneo dogo sana la madini la Mererani Hills, sehemu pekee ambayo madini hayo yanapatikana duniani.
No comments :
Post a Comment