UTEUZI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:-
1. Bibi Bihindi Nassor Khatib ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA).
2. Bibi Asha Ali Abdulla ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA).
3. Bibi Siajabu Suleiman Pandu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
4. Bwana Juma Nyasa Juma ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ.
Uteuzi huo unaanza leo tarehe 21 Julai, 2020.
No comments :
Post a Comment