zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, November 29, 2020

CANADA KUINGIZA WATU ZAIDI YA MILIONI 1 ILI KUIMARISHA UCHUMI!

Kwa maelezo zaidi gonga hapa:
Katika kipindi cha miaka mitatu ijayo nchi ya Canada imepanga kuchukua wahamiaji zaidi ya milioni moja laki mbili ili kujaza mapengo ya upungufu wa watu kwenye maeneo mbalimbali na viwandani na ili kudhibiti kukua kwa uchumi wake.
Waziri wa Uhamiaji Marco Mendicino akitangaza mpango huo amesema mwaka 2021 watahitajika watu 401,000 wakati mwaka 2022 hitajio ni watu 411,000 na mwaka 2023 ni watu 421,000.

Mwaka huu 2020 kufikia mwezi Agosti ilikuwa imeshawapatia ruhusu kuingia nchini humo watu 128425.
Uhamiaji huo umegawanywa kwenye makundi maalum kuanzia wa mwanzo wenye jamaa zao wa kifamilia waliotangulia huko na kundi la mwisho ni aina ya watu wenye shida za kuhama nchini mwao kutokana na adha za kisiasa na mfano wake.

Kutokana na janga la Corona lengo la mwaka huu la watu 341,000 huenda lisifikiwe.


No comments :

Post a Comment