dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, January 19, 2021

ZAWA (UK) YAWASHUKURU AKINA MAMA WA LEICESTER KWA MSAADA WAO!


Jumuiya ya msaada ya Wazanzibari wanaoishi Uingereza ijulikanayo kama ZANZIBAR WELFARE ASSOCIATION - ZAWA (UK) imewashukuru akina mama wa mji wa Leicester (East Midlands) kwa mchango wao wa Sterling 1090 kusaidia kununua vifaa kwaajili ya wenye ulemavu Zanzibar.

Katika mchango wao huo, akina mama hao wameagiza kuwa wapatiwe msaada wale waliopata mitihani katika uchaguzi wa Zanzibar wa 2020.

Kutokana na pesa hizo ZAWA imeweza kununua wheelchairs 15 pamoja na Crutches 17. Vitu vyote hivyo vitasafirishwa kwa haraka sana ili viwafikie walengwa hapa Zanzibar bila ya kuchelewa.

Hii sio mara ya kwanza kwa ZAWA kupeleka Zanzibar vifaa vya kuwasaidia walemavu. Kutokana na imani na moyo wa kusaidia wa Wazanzibari waishio Uingereza, ZAWA pamoja na Hilmy Disability Foundation tokea June 2016 washapeleka Zanzibar Wheelchairs 2000, magodoro 200 na crutches 469.

Blog la Zanzibar Ni Kwetu linawapa hongera akina mama wa Leicester kwa moyo wao wa kusaidia kwa kuwakumbuka ndugu zao huku Zanzibar na pia blog linawashukuru Wana-Jumuiya wote wa ZAWA na Hilmy Disability Foundation kwa kuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia walemavu hapa Zanzibar.

No comments :

Post a Comment