Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza siku saba za maomboezo nchini Kenya kufuatia Kifo cha Rais Magufuli na bendera zitapepea nusu mlingoti, Kenyatta ametoa pole pia kwa Mama Janeth na Watanzania wote kwa ujumla.
“Nimempoteza rafiki, nimempoteza Kiongozi mwenzangu na Kenya tunasimama imara na wenzetu Watanzania kwenye wakati huu mgumu, nimeongea na Mama Samia nimempa pole na kumuhakikishia tunasimama nae pamoja kwenye wakati huu mgumu,” Rais Kenyatta.
Amesema alikuwa akishirikiana kwa karibu na Rais Magufuli na kuongeza kuwa amepoteza ndugu, rafiki na Kiongozi mwenzake.
“Ninakumbuka mara nyingi tulikutana na kuongea kuhusu maendeleo ya nchi zetu mbili, safari yake rasmi alipotembelea Kenya tulifungua barabara na pia alinipatia heshima kubwa sana kwa kumtembelea mama yangu na pia alinialika Tanzania ambapo na mimi pia nilipata fursa ya kutembelea Chato na kuonana na mama yake na tulilala pale nyumbani kwake na kufanya mazungumzo ya kina kuhusu uhusiano wetu kama wanachama wa Afrika Mashariki.”-Kenyatta
Amesema Kenya iko pamoja na Tanzania katika kuomboleza msiba huo mkubwa na itaendelea kushirikiana na Tanzania hadi siku ya kupumzishwa kwa Dkt Magufuli katika nyumba yake ya milele.
“Asubuhi ya leo nilipata nafasi ya kungea na Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na kumpa pole na kumhakikishia kwamba tutaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania hadi kuhakikisha kwamba tumempuzisha rafiki yetu na kuendela na msimamo wake wa kuunganisha wananchi wa Afrika Mashariki,” amesema Rais Kenyatta.
Rais Kenyatta ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ametangaza siku saba ya maombolezo kitaifa nchini Kenya kwa heshima ya hayati Rais John Magufuli.
Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Bendera ya Kenya zitapeperushwa nusu mlingoti katika majengo yote ya serikali nchini Kenya na katika balozi zake nje ya nchi, hadi siku Magufuli atakapozikwa.
GPL
No comments :
Post a Comment