Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
akiongoza Baraza la Mawaziri kwa Mara ya Kwanza baada ya kuapa Ikulu
jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2021
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa shughuli za mazishi ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli zitafanyika Chato Machi 25, 2021 na kusema siku hiyo itakuwa ni siku ya mapumziko.
Rais Samia amesema hayo leo Ijumaa, Machi 19, 2021, wakati akilihutubia taifa mara baada ya kula kiapo cha kuwa Rais Tanzania Ikulu jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Rais Magufuli na kwamba ametangaza kuwa na maombolezo ya siku 21.
“Mipango ya mazishi ni kwamba Jumamosi, Machi 20, 2021, mwili wa Hayati Dkt. Magufuli utatolewa Hospitali ya Jeshi Lugalo na kupelekwa Kanisa la St. Peter’s Oysterbay kwa Ibada na baadaye utapelekwa Uwanja wa Uhuru kwa kuagwa na viongozi.
“Machi 21, 2021, wananchi wa Dar es Salaam wataaga mwili wa Hayati Dkt John Magufuli na baadaye utapelekwa Dodoma.
Machi 22, mwili utaagwa na wananchi wa Dodoma na itakuwa siku ya mapumziko.
Machi 23, mwili utaagwa Mwanza na kupelekwa Chato.
“Machi 24, 2021 ni siku ambayo wanafamilia na wananchi wa Chato na maeneo ya jirani wataaga mwili wa Hayati Dkt. Magufuli.
Machi 25, shughuli ya maziko itafanyika baada ya Ibada kanisani Chato, na siku hii pia itakuwa ni mapumziko.
No comments :
Post a Comment