Ubalozi wa Tanzania nchini Canada umejisogeza zaidi kwa Watanzania wanaoishi Canada kwa kutoa simu ya kiganjani ambayo afisa wa ubalozi atakuwa anayo 24/7.
Japokuwa zipo njia tele za kuwasiliana na ubalozi lakini njia hii ya simu ya kiganjani imewafurahisha wengi, kwani huko nyuma kuupata ubalozi nje ya wakati wa kazi kwa dharura yoyote ile ilikuwa ni shida.
Muakilishi wa blog la ZanzibarNiKwetu jijini Toronto alichukuwa jukumu la kuipiga namba hio nje ya wakati wa kazi ili kuona kama kweli inafanyakazi na kama itapokewa kwa haraka.
Simu ililia mara moja tu na ikapokewa na mfanyakazi wa ubalozi ambae alijitambulisha kama ni Bi Aziza Bukuku. Baada ya blog la ZanzibaNiKwetu kujitambulisha kwa bi Aziza, blog lilichukuwa nafasi hio kutoa hongera kwa ubalozi kwa kufikiria njia hii ya uhakika ya kuwasiliana na Watanzania wa Canada.
Blog likamuhakikishia Bi Aziza kuwa litaisambaza namba hio ambayo ni (1) 613 240 2707 kwa Watanzania wote wanaoishi Canada. Namba hio pia itawekwa kwenye website ya Ubalozi.
Ubalozi inawaomba Watanzania wote wanaoishi Canada kuisambaza namba hio kwa Wana-Diaspora wote kutoka Tanzania, ili wanapotaka kuwasiliana na ubalozi kwa wakati wowote ule na kwa dharura yoyote ile wasipate taabu.
Contacts nyengine za ubalozi wa Tanzania nchini Canada ni kama zinavyoonekana hapa chini.
Tanzanian High Commission in Ottawa, Canada
Ottawa, ON K1N 8J4
Canada
(+1) 613 232 1500
No comments :
Post a Comment