dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, July 19, 2021

UCHAGUZI WA KONDE, PEMBA - ACT WAZALENDO WAJAJUU!

HUJUMA ZA CCM, DOLA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KATIKA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KONDE
Chama cha ACT Wazalendo kinatoa taarifa kuwa matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika uchaguzi wa Jimbo la Konde uliofanyika tarehe 18 Julai, 2021 ni ya kupikwa. Matokeo halisi yanayotokana na kura halisi zilizopigwa na kuhesabiwa yanaonesha kuwa ACT Wazalendo kiliongoza kwa kupata kura 1871 sawa na asilimi 66%

Matokeo halisi ya Vyama vingine ni kama ifuatavyo;-

CCM Kura 1007 Sawa na Asilimia 36%

CHADEMA Kura 211 Sawa na Asilimia 7.5%

CUF Kura 77 Sawa na Asilimia 2.7%

NRA Kura 1 Sawa na Asilimia 0

Demokrasia Makini Kura 2 Sawa na Asilimia 0.1

CCK Kura 3 Sawa na Asilimia 1%

ADA TADEA Kura 1 Sawa na Asilimia 0

NCCR MAGEUZI Kura 4 Sawa na Asilimia 0

SAU Kura 3 Sawa na Asilimia 0

TLP Kura 0 Sawa na Asilimia 0

UPDP Kura 0 Sawa na Asilimia 0

Baada ya kura kupigwa na kuhesabiwa, Mawakala wa ACT Wazalendo walitolewa vituoni bila kupewa nakala za matokeo halisi kisha NEC, ikishirikiana na vyombo vya dola na CCM wakapindua matokeo na kuipa ushindi CCM.

Chama chetu kimesononeshwa sana na dhulma iliyofanyika Konde. Kamati ya Uongozi Taifa inakutana kwa dharura kujadili dhulma hii iliyofanywa kwa Chama chetu na Wananchi wa Konde ili kupata hatua sahihi za kuchukua.

Salim A. Bimani, Kaimu Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar.

19 Julai, 2021.

No comments :

Post a Comment