Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 17, 2021

SHAIRI: BIDADA AMUELEZA FATUMA..." YALIYOPITA SI NDWELE, SISI TUGANGE YAJAO"!

Nimefurahi Fatuma, kuona umetulia,
Moyo umekua mwema, maneno umesikia,
Tumshukuru Karima, dhiki kukuondolea,
Yaliyopita sindwele, sisi tugange yajayo.


Neema iko njiani, karibuni itafika,
Itatoka mawinguni, kwa hariri itashuka,
Itakufata nyumbani, useme unachotaka
Yaliyopita si ndwele sisi tugange yajayo.

Yajayo yafurahisha, Fatuma hujasikia?
Yakale yanatapisha, sipendi kuyarudia
Mimi naona yatosha, yaende yalotokea
Yaliyopita si ndwele sisi tugange yajayo

Hamu yangu kubwa sana, utakapofanikiwa,
Nawe ukapata bwana, Fatuma ukachumbiwa,
Mahari mkapeana, na harusi kufanyiwa,
Yaliyopita si ndwele sisi tugange yajayo.

Furaha yako ni yangu, siku ukiwa harusi
Wewe kama ndugu yangu, mekupenda yangu nafsi,
Taleta kichango changu, usiwe na wasi wasi
Yaliyopita si ndwele sisi tugange yajayo.

Ila kuna jambo moja, nakhisi litanikwaza,
Kua na wewe pamoja, harusini kukufunza,
Hii sio njema hoja, hasada inaeneza,
Yaliyopita si ndwele,sisi tugange yajayo.

Mambo hayo ni zamani, dini haikua pana,
Lakini sasa vyuoni, watu wanasomeshana,
Mume na mke chumbani, watosha kuelimishana,
Yaliyopita si ndwele sisi tugange yajayo.

Kuhusu kuja Canada, wewe usijali sana,
Kwa hio haina shida, mawazo tutapeana,
Ila bwana ndio tenda, inayotutesa sana,
Yaliyopita si ndwele siai tugange yajayo.

Sasa natutulizane, matokeo tusubiri,
Na dua zetu tusome, na hata swala za siri,
Tujikaze tupambane, tumwombe sana kahari,
Yaliyopita si ndwele sisi tugange yajayo.

Bidada/Toronto, Canada, November 17, 2021.


No comments :

Post a Comment