NIFANYE NINI JAMANI,
ENYI NDUGU WALIMWENGU!
Ni mimi tena Fatuma, narejea ukumbini,
Furaha imenihama, majonzi tele kichwani,
Nawaomba ushauri, enyi ndugu walimwengu.
Nalia ndugu nalia, nani afute machozi,
Mwenyewe najikalia, kujinyanyua siwezi,
Hii yangu familia, imejaa wachochezi,
Nawaomba ushauri, enyi ndugu walimwengu.
Hii yangu familia, imejaa wachochezi,
Kaka, babu, bibi pia, pamoja na mashangazi,
Wote wanigeukia, kunitia jinamizi,
Nawaomba ushauri, enyi ndugu walimwengu.
Kwanza walikusudia, nisiolewe Omani,
Ndo wakanisingizia, harusi sina jamani,
Mwanamme kakimbia, bila kuingia ndani,
Nawaomba ushauri, enyi ndugu walimwengu.
Jana wamleta KAKA, Forodhani kule kwangu,
Na yeye akanitaka, nivunje harusi yangu,
Kuwa eti wanashaka, na huyu Faruki wangu,
Nawaomba ushauri, enyi ndugu walimwengu.
Huyu kaka ndio kaka, kaka alienilea,
Kanichukuwa hata mwaka, sijaanza kutimia,
Nilisoma Amerika, yeye alinilipia,
Nawaomba ushauri, enyi ndugu walimwengu.
Wao kubwa yao shaka, ni kutoingia ndani,
Wasema sio dhihaka, kwa kijana wa Kojani,

Aweza kuacha vodka, lakini si biriani,
Hivi sasa wanahoji, juu ya shamba la miwa,
Huyu mtu mwekezaji, vipi hajalinunuwa?
Huyu mtu mwekezaji, vipi hajalinunuwa?
Walikuja wapimaji, na pesa akazitowa
Nawaomba ushauri, juu ya harusi yangu.
Nawaomba ushauri, juu ya harusi yangu.
Pia wamsingizia, kuwa anavuta bangi,
Kwa hii ya leo dunia, wasingeolewa wengi,
Wote wanajivutia, hata na kula mirungi,
Nawaomba ushauri, enyi ndugu walimwengu.
Wamwita Kono la Chuma, hatoi hata shilingi,
Nina yangu taaluma, nafanya kazi Air Wingi,
Siendi kwake kuchuma, kupata mipesa mingi,

Na huko kuoa wengi, ni kutimiza yake sunna,
Kwani tupo kila rangi, na wengine wakichina,
Akiweza ya msingi, naona sababu sina,
Nawaomba ushauri, enyi ndugu walimwengu.
Kwani tupo kila rangi, na wengine wakichina,
Akiweza ya msingi, naona sababu sina,
Nawaomba ushauri, enyi ndugu walimwengu.
Faruki amekubali, kupika na kufagia,
Hatopika tu ugali, na wali wa nazi pia,
Kama sijamkubali, nani atanipikia?
Nawaomba ushauri, enyi ndugu walimwengu.
Tamati ndio nakoma, na ushauri nataka,
Nyote mlionisoma, nisaidiwe haraka,
Niamue yangu hatma, au nimsikize KAKA???
Nawaomba ushauri, enyi ndugu walimwengu.
Niamue yangu hatma, au nimsikize KAKA???
Nawaomba ushauri, enyi ndugu walimwengu.
Fatuma binti Faki/Zanzibar, November 12, 2021.
No comments :
Post a Comment