Fatuma kajizingue, ujiondoshe nuhusi,
Mito saba kazamie, utoke yote mikosi,
Na YASINI jisomee, na aya zote za kursi,
Allah afanye wepesi, nawe upate olewa.
Yu njiani mume mwema, Mola alokwandikia,
Hao wanokuja wima, wote ni wapita njia,
Pengine wote si wema, ndo mana wamekimbia,
Allah afanye wepesi, nawe upate olewa.
Hapo atakapokuja, na wewe utamjua,
Hatokufanyia hoja, na ndani ataingia,
Yeye mekujia moja, na ndilo litalokua,
Allah afanye wepesi, nawe upate olewa.
Kwa mimi wangu uoni, naona usighumiwe,
Nenda kwa wanavyuoni, hizo dua usomewe,
Na huku omba moyoni, nuhusi ziondolewe,
Allah afanye wepesi, nawe upate olewa.
Nasaha zangu ni fupi, ila umenielewa,
Sitaji yupi na yupi, waliokuharibia,
Ila...ukija tena mshipi, mara hii utavua,
Mito saba kazamie, utoke yote mikosi,
Na YASINI jisomee, na aya zote za kursi,
Allah afanye wepesi, nawe upate olewa.
Yu njiani mume mwema, Mola alokwandikia,
Hao wanokuja wima, wote ni wapita njia,
Pengine wote si wema, ndo mana wamekimbia,
Allah afanye wepesi, nawe upate olewa.
Hapo atakapokuja, na wewe utamjua,
Hatokufanyia hoja, na ndani ataingia,
Yeye mekujia moja, na ndilo litalokua,
Allah afanye wepesi, nawe upate olewa.
Kwa mimi wangu uoni, naona usighumiwe,
Nenda kwa wanavyuoni, hizo dua usomewe,
Na huku omba moyoni, nuhusi ziondolewe,
Allah afanye wepesi, nawe upate olewa.
Nasaha zangu ni fupi, ila umenielewa,
Sitaji yupi na yupi, waliokuharibia,
Ila...ukija tena mshipi, mara hii utavua,
Allah afanye wepesi, nawe upate olewa.
Nasubiri mualiko, Fatuma ukishavua,
Kama hujui niliko, namba nitakutumia,
Nione harusi yako, na mume atokuoa
Allah afanye wepesi, nawe upate olewa.
Nasubiri mualiko, Fatuma ukishavua,
Kama hujui niliko, namba nitakutumia,
Nione harusi yako, na mume atokuoa
Allah afanye wepesi, nawe upate olewa.
Bidada/Toronto, Canada, November 12, 2021.
No comments :
Post a Comment