Baada ya video clip ya hapa juu kutoka kwenye channel ya blog la ZanzibarNiKwetu blog limepokea simu kadha kutoka kwa Wa-Tanzania ambao hawaishi Marekeni na ambao wameguswa na hali ya ndugu yetu Daud na wanataka kumsaidia, lakini hawana contacts za Ndugu Daud. Hao ndugu zake na marafiki zake aliowataja kwenye clip pia contacts zao hazijulikani.
Tunakuomba Ndugu Daud uache hapa contacts zako ili wasamaria wema wapate kutabaruku.
Pia, blog limeulizwa kama Ndugu Daud unataka msaada ili uendelee kukaa Marekani au unataka msaada ili urudi nyumbani?
Ndugu Daud alikuwa na maisha ya kujitegemea, lakini yaliyomkuta hivi sasa yoyote kati yetu yanaweza kumfika na kwahivyo ni wajibu wetu kumsaidia ndugu yetu!


Daud toa contacts zako ili upate msaada.
ReplyDelete