Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 8, 2013

HESLB kutumia M-Pesa kukusanya marejesho

NA MWANDISHI WETU

8th October 2013







                               


Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu  (HESLB) imetangaza kuanza kutumia huduma ya M-pesa katika kukusanyia marejesho ya mikopo kutoka kwa wanufaika  ikiwa ni katika mikakati ya bodi ya kuimarisha makusanyo ya urejeshaji wa mikopo hiyo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi, Asangye Bangu alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo mpya na kwamba bodi inaendelea kujipanga kuhakikisha inaboresha njia za urejeshaji mikopo ili kuwapatia walengwa urahisi.

Alisema  mojawapo ya kazi za Bodi ni kusimamia utoaji wa mikopo kwa wanafunzi waliodahiliwa kwenye vyuo vya elimu ya juu pamoja na urejeshwaji wa mikopo iliyotolewa na Serikali kwa waliokuwa wanafunzi wa elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 mpaka sasa kwa nia ya kuufanya mfuko wa Elimu ya Juu kuwa endelevu.

Bingu alisema bodi ina imani kuwa M-pesa itawapatia urahisi wanufaika kuweza kutimiza wajibu wao kisheria wa kurudisha mikopo waliopatiwa kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu.

Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom, Salum Mwalim alisema kuzinguliwa kwa huduma hiyo ni mwendelezo wa jinsi ambayo huduma ya M-pesa inavyorahisisha miamala nchini kuzidi kuwa rahisi.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment