Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 3, 2013

Kitanzi kwa Zanzibar

Written by   //  10/09/2013  //  Makala/Tahariri  //  Zima maoni

DSC03056
SIMPLE MAJORITY?
Hivi karibuni Bunge la Jamhuri ya Muungano lilifanya mabadiliko ya Sheria ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kukawa na ususiaji wa Wabunge wa Upinzani na hata kuzusha tafrani kubwa.
Wabunge wa Upinzani walipotoka mabadiliko hayo yalipitishwa lakini wananchi wengi hawajui athari kubwa inayotokana na upitshaji huo ambao kwa kweli ni kitanzi kwa Zanzibar na kwa demokrasia kwa ujumla.
Hoja kubwa ya Wabunge wa Upinzani ilikuwa ni kwamba Muswada huo ulipaswa kujadiliwa hadharani huko Zanzibar na jambo hilo halikufanywa, sasa ndio inaanza kudhihirika ni kwa nini kulikuwa na umuhimu huo.
Andiko hili fupi litapitia mambo mawili makubwa yaliojitokeza kwenye mabadiliko hayo, ambapo baada ya kutoka Wapinzani,
wale Wabunge wa CCM na wachache wa Upinzani waliobakia hawakuenda kwa kina kifungu kwa kifungu kufanya wajibu wao ila ilikuwa ni kupopoa dhidi ya Upinzani.
1. Suala la kupiisha maamuzi
Kwa mujibu wa Sheria ilipokuwa hapo mwanzo ni kuwa katika Bunge la Katiba uamuzi wa kupitisha Katiba inayopendekezwa ungefanywa kwa kupatikana 3/2 (Thuluthi Mbili) ya Wajumbe wa Zanzibar peke yao na Wajumbe wa Tanzania Bara peke yao.
Kwa maana nyengine uamuzi wowote wa kifungu kwa kifungu lazima upate sauti hiyo ya kila upande na pia kwenye uamuzi wa Katiba inayopendekezwa kwa jumla.
Ila mabadiliko mapya yanataka kuwa baada au itokeapo kuwa hiyo 3/2 ikikosekana basi kifungu au kura ile ya jumla ipitishwe kwa kura ya kawaida yaani Simple Majority.
Hii itakuwa na madhara makubwa kwa Zanzibar lakini pia kwa demokrasia na hasa ni kiza kwa kupitishwa kwa kitu kizito kama katiba ya nchi.
Lakini baya zaidi ni kule kuwepo kwa hiyo kura ya Simple Majority kunaifanya ile kura ya 2/3 isiwe na maana yoyote. Hii inatokana na hakuna ataejali kutafuta suluhu (consensus building) baina ya pande mbili na kwa vifungu vilivyokwama, kwa kujua kuwa hatimae jambo hilo litapita tu kwa Sinmple Majority.
Hii ni hatari kwa Zanzibar, ambayo pia inagawika mno kisiasa baina ya Wazanzibari wenyewe.
2. Kuuliwa kwa Tume ya Katiba
Awali kabisa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipangwa kumaliza muda wake April 2014 baada ya Katiba Mpya kutangazwa. Hili lina umuhimu mkubwa kwa sababu kuwepo kwa chombo hicho kunajenga usalama wa mfumo huo mzima.
Tume ya Katiba pia kwa Sheria ilivyokuwa ilikuwa imepewa wajibu wa kuendesha elimu ya umma katika kipindi kabla ya Kura ya Maoni.
Lakini kwa mujibu wa mabadiliko ya Sheria yaliofanywa, Tume ya Katiba inavunjwa mara baada ya kuwasilisha Rasimu ya Pili kwa Bunge la Katiba.
Utata unakuja katika mambo yafuatayo:
a) Bunge hilo la Katiba limepewa mamlaka ya kumwita Mwenyekiti, Makamo au Mjumbe yoyote kutoa ufafanuzi wa jambo lolote, ila suala litakuwa huyo Mwenyekiti, Makamo au Mjumbe wataitwa kwa cheo gani?
b) Umuhimu wa kuwepo Tume ni kuwa ni kiungo na kushauri, kama itakuwa haipo Bunge la Katiba itakuwa ina maana inafanya kila kitu katika hali ya “upya” kabisa.
c) Kama Tume itavunjwa pia kitengo chake madhubuti cha wataalamu na rekodi zake zote hazitaweza kuwa na usaidizi kwa Bunge la Katiba na kwa hivyo Tume itakuwa inaelea.
Ni fikra yangu kuwa huu ndio wakati muwafaka kwa Vyama vya Upinzani kukusanya nguvu zao pamoja kulisimamia jambo hili la Mabadiliko hayo kwa umuhimu mkubwa kwa :
i) Kufanya uchambuzi wa kina
ii) Kuwasiliana na umma wa Tanzania
iii) Kufanya ushawishi wa kisiasa
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment