NA MWANDISHI WETU
4th October 2013

Ushauri huo ulitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki mpya ya Maendeleo, Ibrahim Mwangalaba, wakati akielezea umuhimu wa hisa na maendeleo.
Alisema kwa kutambua umuhimu huo, benki hiyo inatarajia kusajili hisa zake DSE na kuwawezesha Watanzania kuzimiliki.
Benki yetu imesajiliwa katika soko la Hisa na Mitaji na hivyo kuwa ni benki ya kwanza nchini kuanza biashara na kusajiliwa moja kwa moja katika soko hilo.
Hivi sasa jumla ya hisa milioni nane zinauzwa katika soko la awali kwa bei ya Sh. 500 kwa hisa.
Alidokeza kuwa baada ya uuzaji wa hisa za Maendeleo Bank kufikia ukomo Oktoba 15, mwaka huu, Benki ya Maendeleo itatangazwa rasmi kuwa moja kati ya taasisi zitakazokuwa kwenye soko la DSE.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment