Hatimaye Sheikh Azzan Khalid Hamdan ameondoka leo mchana kuelekea nchini India kwa matibabu.
Sheikh Azan amesema anawashukuru wote waliofanikisha safari yake kwa michango yao ya hali na mali na kuwataka kumwombea dua katika kipindi chote cha matibabu.
“Nashukuru kwa ujumla, nawaomba wale wote walionichangia na kufanikisha safari yangu, InshaaAllaah Mwenyezi Mungu atawalipa, pia naishukuru sana familia yangu kwa kuwa na mimi katika kipindi chote tangu nilipoachiwa kwa dhamana’ amesema Sheikh Azzan.
Sheikh Azzan ameondoka kwa ndege ya Oman Air saa saba mchana.
Maelezo na Munir Zakaria
Via Zanzinews
No comments :
Post a Comment