Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, May 13, 2015

JK aingilia kati mafuriko dar

Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete amengilia kati mafuriko yaliyolikumba Jiji la Dar es Salaam kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha vifo vya watu 12, kuwakosesha wengine makazi na kuharibu miundombinu.
 
Jana Rais Kikwete alitembelea maeneo kadhaa yakiwamo ya Mbagala Kuu wilayani Temeke na Jangwani wilayani Ilala ambayo yameathirika kutokana na mvua hizo.
 
Rais Kikwete, ambaye aliambata na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raimond Mushi na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, aliliagiza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kujenga daraja la muda linaliunganisha wakazi wa Mbagala Kuu na Kunduchi, ambalo lilikatika kutokana na mvua hizo.
 
Kutokana na daraja hilo kubomoka, wakazi wa maeneo hayo wamekosa mawasiliano.Aidha, Rais Kikwete, aliwaagiza Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kupitia kwa mwakilishi wake, Elisos Mtenga, kusafisha mto Msimbazi kwa kuzoa taka zote na kuondoa mchanga uliojaa na kusababisha maji kushindwa kupita.
 
“Serikali haiwezi kuliagiza JWTZ kuja hapa kuzoa mchanga na taka ambazo zimejaa wakati hii ni kazi ambayo Tanroads mnaweza kuifanya. Hizi taka zilizojaa ndizo zinazosababisha maji yanashindwa kupita. Kwanini mnashindwa kusafisha, ina maana hamna maarifa?” alihoji Rais Kikwete.
 
Alisema ni vyema wakaondoa taka hizo ambazo zinaonekana kikazwo kwa kuzuia maji mengi yasipite chini ya daraja na kupita juu ya daraja. 
 
Alisema kwa kufanya hivyo, mafuriko yatadhibitiwa katika eneo hilo.
 
KUZUNGUMZIA ATHARI KESHO
Rais Kikwete aliahidi kuzungumzia hali ya mafuriko yaliyotokea katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam kesho, baada ya kuhitimisha ziara ya kutembelea maeneo hayo.
 
Rais Kikwete aliahidi kutembelea pia katika maeneo ya Magomeni Hananasif na Tegeta kesho.
 
MABONDENI WAATHIRIKA TENA.
Katika hatua nyingine, baadhi ya wakazi wanaoishi maeneo ya mabondeni jijini Dar es Salaa wameathirika tena, baada ya mvua kuongezeka tena juzi na jana, hivyo maji kuingia kwenye makazi yao.
 
NIPASHE jana lilishuhudia wakazi wa maeneo ya Jangwani ambao walishaanza kurejea kwenye makazi yao baada ya mvua kukatika, wakianza kuhamisha vitu vyao upya kwa ajili ya kutafuta hifadhi.
 
Wakazi hao walikutwa wakiwa wamekusanyika katika eneo la karavati lililoko katika barabara ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi (Dart) huku wakiwa na magodoro pamoja na nguo.
 
Hali hiyo ni tofauti na iliyokuwa juzi NIPASHE lilipowakuta wakazi hao wakiwa wamepungua katika eneo hilo na na wachache wakiendelea na usafi kwenye nyumba zao tayari kurejea katika makazi yao yaliyozingirwa na maji ya mvua za awali.
 
Shabani Manyimbo, aliliambia gazeti hili kuwa, tayari walikuwa wameanza kurejea kwenye makazi yao.
 
“Kama unavyoona, haya maji ni mengi na tayari yameingia kwenye makazi yetu, imebidi tuondoke kwani yanaweza kujaa tena ghafla na kusababisha maafa,” alisema Manyimbo.
 
Pia katika karavati la daraja la Jangwani wafanyabishara ndogo ndogo kama wauza vinywaji na chakula walionekana wakiwauzia wakazi hao bidhaa mbalimbali.
 
Kadhalika, karavati hilo lilikuwa na nguo ambazo wakazi hao waliziweka kujikinga na mvua.
 
MTO MSIMBAZI WAWATISHA WAKAZI KIGOGO
Katika maeneo ya Kigogo, NIPASHE lilishuhudia maji yakiingia ndani ya nyumba za makazi na mengine kuzagaa barabarani.
 
Mto huo ulijaa maji na mengine kuingia kwenye makazi ya watu hali iliyowafanya wakazi hao kupatwa na hofu.
 
Baadhi ya waathirika wakizungumza na NIPASHE walisema maji yalikuwa yameanza kupungua na kuanza kusafisha nyumba zao na kupata matumaini ya kurejea katika makazi yao, lakini mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia jana ilisababisha waanze kuishi kwa hofu, alisema Zuberi  Khamisi.
 
Subira Majaliwa, mkazi wa  Kigogo Mji mpya, alisema: “Mvua hizi zinazonyesha zimenitia hasara kubwa, kwani siwezi kwenda kufanya biashara yangu ya kupika maandazi huku nikitakiwa kununua magodoro mapya.” 
 
Katika maeneo ya Tabata Matumbi, Mgomeni, Msasani Bonde la Mpunga na Sinza maji yalijaa barabarani hali ilioyosababisha foleni ya magari kwenye maeneo hayo. 
 
SERIKALI: YASEMA HAKUNA MSAADA 
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raimond Mushi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, alisema msimamo wa serikali uko pale pale kwamba haitatoa msaada kwa waathirika wa mafuriko kwani walishatakiwa kuondoka katika maeneo hayo kabla ya mvua.
 
Alisema serikali itakacho kifanya ni kutoa matibabu kwa waliopata madhara, kuokoa waliozama na kuboresha miundombinu.
 
“Msimamo wa serikali hauwezi kubadilika kama ambavyo mkuu wa mkoa, Said Meck Sadiki, alivyokwisha sema, hatutatoa msaada wala fidia kwa watu wanaoishi mabondeni,” alisema Mushi.

CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment