Avuna kura za `Ndiyo` 269 sawa na asilimia 98.2
Wabunge wengi CCM, Chadema watetea nafasi zao.jpg)
Licha ya kupita kwa kishindo, wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi huo, walimpigia Mbowe kura tano za kumkataa.
Akitangaza matokeo, Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Kaskazini na Mbunge wa Karatu, Mchungaji, Israel Natse alisema: " Mbowe aliyekuwa mgombea pekee wa nafasi ya ubunge, alipigiwa kura za ndiyo 269 sawa na asilimia 98.2, lakini pia alipigiwa kura tano za hapana na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Kura ya Maoni."
Akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa mkutano huo, kuhusu haki ya kikatiba ya wajumbe wa mkutano huo kupiga kura ya hapana; Mchungaji Natse alisema kuwa kura za kumkataa zilitokana na kukua kwa demokrasia ndani ya chama hicho kinachojiandaa kushika dola baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.
Katika uchaguzi huo uliofanyika katika mji mdogo wa Bomang'ombe, wajumbe halali waliopaswa kushiriki zoezi hilo walikuwa 274 kutoka Kata zote za Wilaya hiyo.
Hata hivyo; akizungumza muda mfupi baada ya kutangazwa matokeo hayo, Mbowe alisema,"Nawashukuru sana wajumbe kwa kuniamini na kunipa heshima ya kuendelea kutetea ubunge wa Hai na pia kuendeleza mapambano dhidi ya utawala wa CCM. Nawahakikishia kwamba nitashinda tena kwa kishindo na moto watauona mwaka huu."
Mbowe alisema sababu ya yeye kuendelea kupigania ukombozi wa nchi kutoka mikononi mwa CCM ambayo imewagawa Watanzania katika makundi ya walionacho na wasionacho, hakuwezi kumfanya asiwaze juu ya ukombozi wa fikra na maendeleo ya kweli dhidi ya umma wa Watanzania.
GEITA: VICK KAMATA ATETEA VITI MAALUM
VICK Kamata, amefanikiwa kutetea nafasi yake ya ubunge wa Viti maalum kupitia CCM Mkoa wa Geita, baada ya kuongoza katika kura za maoni kwa kupata kura 426 na kuafuatiwa na Josephine Chagula aliyepata kura 419.
ARUSHA: CATHERINE MAGIGE APETA
Mbunge wa Viti Maalum Vijana (UVCCM), Catherine Magige, ameibuka kidedea kupitia viti maalum Jumuiya ya Wanawake CCM Mkoa wa Arusha (UWT), kwa kupata kura 409 kati ya kura 560 zilizopigwa huku kura tatu zikiharibika. Mshindi wa pili katika matokeo hayo ni Vailet Mfuko aliyepata kura 248, kati ya kura hizo zilizopigwa kumtafuta mwakilishi wa pili.
AMINA MOLEL ASHINDA
Kundi la watu wenye ulemavu: Amina Mollel alishinda kwa kuzoa kura 362 na kumbwaga mwenzake katika kundi la walemavu Christina Manyenye aliyepata kura (196).
TUMWAGILE MWAKYUSA: KUNDI LA WASOMI
Kundi la wasomi: kuwa ni Tumwagile Mwakyusa alipata kura (502) na kumbwaga mwenzake Jesca Njau (51) Nafasi ya kundi la mashirika yasiyo ya kiserikali inawaniwa na Anjela Bayo ambaye hakuwa na mpinzani alipata kura zote 560.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya Chadema, Lazaro Massay, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, amebwagwa katika kinyang’anyiro cha kuwania kuteuliwa kuwa mgombea wa kiti cha ubunge katika kura za moani zilizopigwa juzi.
Alibwagwa na mgombea mwenzake Willy Qhambalo. Qhambalo alishinda kwa kura 217 kati ya kura 302 ambapo mpinzani wake wa karibu Massay alipata kura 81.
MOROGORO: WABUNGE MSAFIRI, ISHENGOMA, SARA WAULA
Wabunge watatu wa Viti Maalumu Sara Msafiri, Dk. Christine Ishengoma na Magreth Mkanga wamefanikiwa kuzitetea tena nafasi zao.
Wabunge hao wamepita kwenye uchaguzi wa kura za maoni wa Umoja wa Wanawake (UWT) kupitia mkoa wa Morogoro.
Dk. Ishengoma alishinda kwa kura 641 kati ya 771 zilizopigwa. Msafiri alichanguliwa kwa kura 608.
Kwa upande wa vyuo vikuu, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe , Dk. Jasmine Bunga, ameshindwa nafasi ya kwanza kwa kupata kura 310.
Katika kinyang’anyiro cha ubunge Viti Maalumu kwa watu wenye ulemavu, mchuano ulikuwa mkali kati ya mtetezi wa kiti hicho Margaret Mkanga ambaye alipata kuwa 424 kati ya 759 zilizopigwa.
Muingizaji wa filamu nchini Wastara Issa, alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 252.
Kundi la Ubunge Viti Maalumu kupitia NGO’s , Christina Kulunge alishinda kwa kura 225.
Kundi la wafanyakazi, mgombea aliyejitokeza alikuwa Mhandisi Vidate Ligalama ambaye alipigiwa kura ya ndiyo kwa kupata kura 651 na 26 za hapana.
DODOMA: Mbunge wa Viti Maalumu, Felister Bura (CCM) amefanikiwa kutetea kiti hicho baada kushinda kura 457. Mshindi wa pili ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Fatuma Toufiq aliyepata kura 368.
Shamsa Mangunga aliambulia kura 25 kati ya kura 728. Hata hivyo uchaguzi huo umedaiwa kugubikwa na vitendo vya rushwa hali iliyosababisha wagombea 19 kati ya 22 kususia kusaini matokeo ya uchaguzi huo.
Kupitia kundi la watu wenye ulemavu, msanii wa muziki wa kizazi kipya Khadija Shaaban maarufu Keisha, aliibuka mshindi kwa kupata kura 340.
Kundi la wasomi aliyeshinda ni Juliana Manyerere, kundi la Asasi zisizo za kiserikali aliibuka Chiku Mugo huku katika kundi la wafanyakazi Mwalimu wa shule ya Msingi Kizota Mwanamanga Mwanduga akishinda nafasi hiyo.
Mmoja wa wagombea hao, Judith Mieya alisema amegomea kusaini matokeo kutokana na kushindwa kukubaliana na hali ya utovu wa nidhamu katika chama chao.
MBEYA: HILDA NGOYE AANGUKA VIBAYA
Mbunge mkongwe wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Hilda Ngoye kupitia CCM, amekuwa mbunge wa kwanza mkoani hapa kupoteza nafasi yake baada ya kuagushwa vibaya kwenye uchaguzi uliofanyika jana jijini Mbeya.
Mbunge wa Viti Maalum, Dk. Mary Mwanjelwa, aliibuka kidedea kwa kura 505 na kuwabwaga wagombea wenzake 11.
Akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya, Mwangi Kundya alisema kuwa kura zilizopigwa zilikuwa 625, kura mbili ziliharibika na kura halali zilikuwa 623.
Aliyemfuata ni Mary Obadia aliyepata kura 192 huku Ngoye akishika nafasi ya tatu kwa kuambulia kura 164.
WABUNGE MBEYA WATETEA NAFASI ZAO
Wabunge wengine wanaoendelea kutetea nafasi zao mkoani Mbeya ni Dk. Harrison Mwakyembe (Kyela), Dk. Ariko Kibona (Ileje), Godfrey Zambi (Vwawa), Mchungaji Luckson Mwanjale (Mbeya Vijijini), Philip Mulugo (Songwe), Victor Mwambalaswa (Lupa) na Dickson Kilufi (Mbarali) wote kupitia CCM, David Silinde (Momba) na Joseph Mbilinyi Maarufu kwa jina la Mr. II Sugu (Mbeya Mjini) kupitia Chadema).
SONGEA: Joseph Fuime ambaye alikuwa diwani wa kata ya Songea Mjini ameibuka mshindi kwa kupata kura 139 kati ya kura 214 zilizopigwa katika kura za maoni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment