Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, July 26, 2015

Simu chanzo cha moto ulioteketeza maduka Mtwara

Image result for fire caused by cell phone

Jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara, limesema uchunguzi wa awali dhidi ya tukio la ajali ya moto lililoteketeza mali zote kwenye duka la Mkuti Pharmacy zenye thamani ya zaidi ya bilioni 1.5,  umebaini kuwa chanzo ni simu ya mlinzi aliyokuwa akiichaji kwenye swichi iliyopo kwenye baraza la jengo hilo.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa mapema wiki hii na kusainiwa na Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Masasi, imeeleza kuwa, soketi ambayo mlinzi huyo, Joseph Masanja, alikuwa akichaji simu, hutumika kuunganisha jenereta, umeme wa Tanesco unapokatika.

Taarifa hiyo imesema kuwa, wamebaini kuwa soketi hiyo hutumika pia kuchajia simu, na siku ya tukio mlinzi huyo alikuwa amefanya hivyo wakati akiendelea kuzungukia lindo lake.

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa wakati akizunguka ndipo moto huo ulipoanza na hatimae kushika maboksi yaliyokuwa yamehifadhiwa eneo hilo.

Kadhalika imesema kuwa, baada ya moto huyo kushika maboksi hayo ulisambaa zaidi na kuunguza maduka yaliyokuwepo hapo.

Tukio hilo la moto lilitokea Julai 15, mwaka huu kata ya Mkuti, tarafa ya Lisekese wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kwenye duka linalomilikiwa na Husseni Kadari.

Moto huo uliteketeza dawa, vifaa tiba vyote vilivyokuwepo dukani humo pamoja na maduka mawili ya nguo yaliyopakana na Mkuti Pharmacy mali ya Mfaume Ajili na Shabani Nalino.

Mali iliyoteketea kwenye duka la Kadari thamani yake ni zaidi ya Sh. bilioni 1.3.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment