dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 24, 2015

Maalim Seif: Muungano kielelezo cha umoja.

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (Cuf), Seif Shariff Hamad.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (Cuf), Seif Shariff Hamad amesifu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuwa ni kielelezo cha umoja na mshikamano wa Watanzania.
 
Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Maalim Seif alisema zipo faida nyingi za Muungano likiwamo suala la usalama na amani katika taifa.
 
Siwezi kusema kwamba hakuna faida katika Muungano... faida zipo, kwa mfano suala la ‘security and stability’ Muungano ni jambo la msingi na lina faida alisema.
 
Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Cuf kwa muda mrefu, alikuwa akijibu swali aliloulizwa na mtangazaji wa Shirika hilo, Zuhura Yunus, aliyemuuliza kuhusu faida ya kuwa na Muungano.
 
Alisema msimamo wake na wa chama chake bado upo pale pale wa kutaka mamlaka kamili ya Zanzibar ndani ya Muungano kwa madai mfumo huo ndio suluhisho la kero za Muungano.Sisi tunasema tunataka mamlaka kamili, alisema, ingawa alipoulizwa kwanini wanaunga mkono rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyopendekeza mfumo wa Shirikisho la Serikali tatu,  alisema yeye na chama chake msimamo wao ni mamlaka kamili, lakini na rasimu wanaiunga mkono.
 
Alisema kuwa licha ya kufanyika kwa vikao vingi vya kuondoa kero za Muungano, hakuna mafanikio ya utatuzi wa kero hizo na ndio maana chama chake kinaushabikia mfumo wa muundo wa Muungano wa Mkataba ambao pia haumo katika sera ya chama hicho. Hadi sasa sera ya chama cha Cuf ni mfumo wa muundo wa Muungano wa serikali tatu, ingawa katika mchakato wa kuandika katiba mpya Cuf walijiunga katika Ukawa wakitetea mfumo wa serikali tatu.
Alisema chama chake kimeanza mchakato wa kumwandaa mwanasiasa ndani ya chama hicho atakayemrithi nafasi yake ya kuwania urais wa Zanzibar na ile ya Katibu Mkuu kwa kuwa utu uzima umeanza kumzonga na kuchoka.
 
Chama chetu kimeshamuandaa mtu mwengine, lakini simtaji nani, lakini yupo wakati ukifika mimi nitastaafu ukatibu mkuu maana kama mwanadamu ninazeeka na kupungukiwa na nguvu hivi sasa sina nguvu kama zile za zamani, alisema.
 
Hii ni mara ya tano katika kipindi cha miaka 20, Hamad akiwania urais wa Zanzibar bila kushinda. Pia amekuwa Katibu Mkuu wa Cuf tangu mwaka 1999.  Kabla ya hapo aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Cuf. 
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment