dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 24, 2015

TAARIFA YA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR MHE. JECHA SALIM JECHA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UCHAGUZI MKUU WA TAREHE 25 OKTOBA 2015



TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR


TAARIFA YA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR 

MHE. JECHA SALIM JECHA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 

25 OKTOBA 2015


Ndugu Wananchi, 


Kesho Jumapili tarehe 25 Oktoba 2015 ni siku ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar 

ambapo wananchi wa Zanzibar watapiga kura kumchagua, Rais wa Zanzibar, 

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani kwa upande mmoja na 

kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge kwa upande 

mwengine. 


Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imekamilisha taratibu zote muhimu 

zitakazowawezesha wapiga kura kupiga kura bila ya usumbufu. Aidha, vifaa 

vyote muhimu vinavyohusika na kazi ya kupigisha kura vimepatikana na

vimeshasambazwa katika vituo vyote vya kupigia kura Unguja na Pemba.


Ndugu wananchi, uchaguzi ni zoezi ambalo hufanyika kwa misingi ya Sheria,

linalohitajia utulivu na usalama wa hali ya juu. Kwa hivyo, siku ya kupiga kura, 

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inawaomba wananchi wote kuzingatia ipasavyo 

maelekezo ambayo yametolewa na yatakayotolewa na Tume ya Uchaguzi katika 

vituo vya kupigia kura, kwani maelekezo hayo yatatolewa kwa kufuata mwongozo 

wa Sheria na yanalenga kudumisha utulivu wakati wote wa kupiga, kuhesabu na 

kujumlisha kura katika vituo. Tume ya Uchaguzi inawasihi wapiga kura wote 

kuwa endapo katika zoezi la upigaji kura kutajitokeza tatizo kwa upande wa vifaa

ni vyema wafuate taratibu za sheria katika kulitafutia ufumbuzi na kamwe 

yasipitishwe maamuzi yanayokizana za sheria.

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inawaomba wananchi kuyafahamu na kuyaelewa 

mambo yafuatayo kuwa:-


1. Upigaji kura utafanyika katika vituo vya kupigia kura ambavyo vitakuwa na 

wastani wa wapiga kura 350. Kila kituo cha kupigia kura kitakuwa na 

Msimamizi ambaye atakuwa ndiye kiongozi na mdhamini wa shughuli za 

uchaguzi katika kituo husika. Pia, kutakuwa na Wasimamizi Wasaidizi wa kituo 

ambao watafanya kazi chini ya dhamana ya Msimamizi wa kituo.


2. Kila mwananchi aliyejiandikisha kuwa mpiga kura kwa uchaguzi wa Zanzibar 

na aliyekuwa na shahada ya kuandikishwa kuwa mpiga kura kwa Uchaguzi wa 

Zanzibar, na ambaye taarifa zake zitakuwemo katika Daftari la wapiga kura 

atakuwa na haki ya kupiga kura kumchagua Rais wa Zanzibar, Mjumbe wa 

Baraza la Wawakilishi na Diwani kwa upande mmoja na kwa upande 

mwengine atapiga kura kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 

Tanzania na Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 


3. Upigaji kura utafanyika katika eneo ambalo mtu amejiandikisha au karibu na 

sehemu hiyo. Katika kila kituo cha kupigia kura kutakuwa na watendaji wa 

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na 

maandishi yanayowaelekeza wapiga kura kujua wapi watapiga kura kwa ajili 

ya kumchagua Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na 

Diwani kwa uchaguzi wa ZEC na Rais wa Jamhuri ya Muungano na Mbunge 

kwa upande wa NEC. Aidha, katika kila kituo cha kupigia kura, kutakuwa na 

mawakala wa vyama vya siasa ambao watakuwa na jukumu la kuwakilisha na 

kulinda maslahi ya wagombea wa vyama vyao katika kituo, kugundua watu 

wanaojifananiza (personation) na kushirikiana na Msimamizi wa kituo na 

Wasimamizi Wasaidizi wa vituo juu ya usimamizi mzuri wa sheria katika kituo.


4. Kuwa vituo vyote vya kupigia kura vitafunguliwa saa 1.00 asubuhi na 

kufungwa saa 10.00 jioni. Muda huo utakapomalizika hakuna mpiga kura 

atakayeruhusiwa kujiunga katika msitari wa kuingia katika kituo cha kupigia 

kura, bali watakaokuwa katika misitari ya kuingia kituoni ndani ya muda huo,

wataendelea na upigaji kura hadi mtu wa mwisho atakapomalizika. Itakapofika 

saa 10 kamili askari atasimama nyuma ya mtu wa mwisho katika mstari. Mtu 

yeyote atayekuja baada ya hapo hataweza kupiga kura.


5. Kila mpiga kura ajitahidi kufika mapema katika kituo cha kupigia kura na 

ahakikishe kuwa amechukuwa shahada yake ya kupigia kura. Na kuwa, iwapo 

atawakuta watu wengine wamejipanga katika mstari, ajipange nyuma yao bila 

ya usumbufu.


6. Wapiga kura wagonjwa na ambao hawawezi kupiga kura wenyewe, 

wanaruhusiwa kwa mujibu wa Sheria kwenda vituoni na watu wanaowaamini 

ili kuwasaidia kupiga kura. Hairuhusiwi na ni marufuku kwa mtu asiyekuwa na 

sifa za kupigiwa kura kupigiwa kura. Endapo itabainika Mkuu wa Kituo cha 

kupigia kura au Msaidizi wake ataruhusu mtu au watu wasiostahiki kupigiwa 

kura hatua za kinidhamu na sheria zitachukuliwa mara moja. Tume inawasihi 

Wakuu wa Vituo na Wasaidizi wao kuwa waangalifu sana na makosa hayo.


7. Hairuhusiwi kuendesha kampeni ya aina yoyote katika vituo vya kupigia kura. 

Na kuwa, si ruhusa kwa mpiga kura au wapiga kura kuvaa sare au alama za 

vyama vyao vya siasa au wagombea wanapokwenda kupiga kura. Aidha, ni 

marufuku kwa wapiga kura kwenda katika vituo vya kupigia kura wakiwa 

wamebeba silaha za aina yoyote kwa njia ya dhahiri au kificho.


8. Mtu yeyote haruhusiwi kubaki kituoni baada ya kupiga kura yake. Hivyo, Tume 

ya Uchaguzi ya Zanzibar inawasihi wapiga kura mara wanapomaliza kupiga 

kura waondoke vituoni na kurejea nyumbani au kwenda katika shughuli zao 

nyengine. Inasisitizwa mzunguuko wa mita mia mbili kutoka kituo cha kupigia 

kura hapatakiwi kuonekana mtu yeyote asiyestahiki.


9. Kila mgombea anaruhusiwa kuweka wakala mmoja katika kituo cha kuhesabia 

kura na kujumlishia kura. Kila wakala wa mgombea atapatiwa nakala ya fomu 

ya matokeo ya hesabu ya kura kituoni baada ya kura kuhesabiwa katika kituo na 

nakala ya fomu ya matokeo ya jimbo au wadi baada ya kura kujumlishwa.


10.Hakuna mtu mwengine yeyote zaidi ya watu waliotajwa katika Sheria ya 

Uchaguzi anayeruhusiwa kuwepo katika eneo la kuhesabia kura. Aidha, hakuna 

mtu zaidi ya waliotajwa katika sheria atakayeruhusiwa kuwepo katika masafa 

ya mita mia mbili kutoka pahala panapohesabiwa kura.


11.Kazi ya kujumlisha na kuhesabu kura kwa wagombea Uwakilishi na Udiwani 

kwa vituo itafanywa katika vituo maalum katika kila jimbo. Katika vituo hivyo,

wagombea wote watakaoshinda kwenye chaguzi hizo (Uwakilishi na Udiwani) 

ndimo watakamotangazwa na Wasimamizi wa Uchaguzi wa majimbo husika.


12.Kazi za kujumulisha hesabu za kura kwa wagombea Urais wa Zanzibar 

zinafanywa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa mujibu wa Sheria, na ni 

Tume ya Uchaguzi peke yake ndiyo yenye madaraka ya kumtangaza mshindi 

wa kiti cha Urais wa Zanzibar baada ya kuthibitisha matokeo ya mshindi.


13.Ni makosa kufanya mambo yafuatayo wakati wa zoezi la upigaji wa kura:-

Kutaka kupiga kura kabla ya kituo hakijafunguliwa au baada ya kufungwa.

Kupiga kura au kukusudia kupiga kura kama huna haki ya kufanya hivyo.

 Kupiga kura au kukusudia kupiga kura zaidi ya mara moja katika uchaguzi 

      mmoja.

 Kupiga kura kwa jina la mtu mwengine, aliyehai, aliyekufa au kwa njia ya 


udanganyifu.


 Kutia ndani ya sanduku la kura kitu chengine chochote zaidi ya kura.

 Kuingiza au kuharibu karatasi ya kura au shahada ya matokeo au fomu 

      yoyote inayohusiana na uchaguzi.

 Kujaribu kumshawishi mpiga kura kumchagua mgombea maalum.

 Kutaka kujua mgombea ambaye mpiga kura anakusudia kumpigia kura au 

      aliyempigia kura.



Ndugu Wananchi na Viongozi wa Vyama vya Siasa cha muhimu kuliko yote 

katika maelezo yangu ni matokeo baada ya zoezi la kupiga na kuhesabiwa kwa 

Katika hilo naomba kuwakumbusha kuwa katika ushindani wowote ule kuna 

kushinda na kushindwa. Hivyo, ni vyema kwa wagombea na wafuasi wa 

wagombea na vyama vyao kuwa tayari kwa matokeo ya ama kushinda au 

kushindwa. Na pale ambapo mgombea hakuridhika na matokeo ni vyema akatumia 

njia au taratibu za kisheria katika kutoa malalamiko yake. Njia nyengine yoyote

mbadala wa hiyo wakati wa kushughulikia maalamiko ya kiuchaguzi inaweza 

kuondoa utulivu na kupelekea hasara kubwa kwa nchi yetu.


Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa upande wake inafanya kila linalowezekana 

katika kuendesha Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa tarehe25 Oktoba 2015 kwa 

salama na amani na pia itahakikisha kuwa Uchaguzi mwaka 2015 unakuwa huru 

na wa haki.


14. Ndugu wananchi imebainika tabia kwa baadhi ya wafuasi wa vyama vya 

Siasa kuwa siku ya kupiga kura au kabla ya hapo kuwanyanganya vitambulisho 

vya kupigia kura wapiga kura wa Chama au vyama vyengine au kuvinunua kwa 

madhumuni ya kuwazuia kupiga kura na eti kupunguza kura za vyama 

vyengine, mara nyengine huwatisha au kuwasusia huduma za kijamii. Hayo ni 

makosa yasiyovumilika. Tume ina waonya watu wote wenye tabia ya aina hiyo 

waache mara moja. Atayebainika na vitendo hivyo atachukuliwa hatua za 

kisheria. Mpiga kura yeyote atayepatwa na kadhia ya aina hizo atoe taarifa 

kwenye mamlaka zinazohusika kama vile Tume yenyewe au Polisi. Vyama vya 

siasa vinaombwa kuwatahadharisha wafuasi wao kutojingiza katika makosa ya

aina hiyo.


Nawatakia wananchi wote wa Zanzibar kila kheri na mafanikio katika upigaji wa 

kura kesho tarehe 25 Oktoba, 2015.


Ahsanteni kwa kunisikiliza.


JECHA SALIM JECHA

MWENYEKITI,

TUME YA UCHAGUZI

ZANZIBAR


No comments :

Post a Comment