KIZAZI CHA DIASPORA KUWANIA NAFASI KATIKA CONGRESS


Will Jawando,mkewe Michell Jawando na watoto wao Alia,Addison and Ava
Will Jawando ni mzaliwa wa Silver Spring,Maryland kwa familia ya Mwanadiaspora 'Jawando' kutoka Nigeria na Mama ambaye ni mwenyeji wa Marekani.
Will amepitia changamoto mbalimbali zilizo katika jamii na hata kumpoteza rakifi yake wa pekee
katika shambulizi la risasi. Jambo hili lilimpelekea kukabidhi maisha yake katika utoaji huduma na
utatuzi wa matatizo ya jamii na kuweka jitihada katika elimu .
Will Jawando alihitimu elimu ya juu na shahada ya Sheria, ambapo aliendelea na utoaji huduma kwa
jamii katika ngazi tofauti hususani; Legislative Staffs House of Democratic chini ya uongozi wa Nancy Pelosi,US- Senator Barack Obama na ngazi nyingine mbalimbali.
Kama Mwanadiaspora ninayetambua changamoto za huduma ya afya kwa wasio na vibali vya kuishi
nchini ,Will Jawando alinigusa zaidi pale aliponieleza kuhusu baadhi ya changamoto za wahamiaji
akisema kuwa, mbali na ukosefu wa hati halali , wahamiaji wote hushiriki katika ulipaji wa kodi na
hivyo kuchangia maendeleo ya Taifa. Swala hili na mengine mengi ni miongoni mwa maswala ambayo
ana nia ya kuyapa kipaumbele.
Will Jadando kupitia Democratic party anasimama katika nafasi ya Congress, kama mtoto
wa Mwana-Diaspora kutoka Afrika na wa pili tokea Mhe. rais Barak Obama.
Mhe rais Barak Obama akisalimiana na familia ya Jawando na kumkaribisha mtoto wao mpya.
Images
willjawando.com
Story;NesiWangu
Story;NesiWangu

No comments :
Post a Comment