
Mbunge wa Jimbo la Busega Mkoani Simiyu, Dk. Raphael Chegeni (CCM), ameiomba serikali ya wamu ya tano ya Rais John Magufuli kuimarisha miundombinu ya kazi katika wilaya na mikoa mipya nchini ili kurahisisha maisha ya wananchi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Dk. Chegeni alisema Busega ni moja ya wilaya mpya ambazo zilitangazwa mwaka 2010 lakini inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, barabara na watendaji.
Alisema lengo la serikali ya kuanzisha mamlaka mpya lilikuwa zuri lakini maeneo hayo yanakabiliwa na changamoto za rasilimali, hivyo ni vyema serikali ikatoa kipaumbele katika kuwezesha wilaya na mikoa hiyo viweze kutoa huduma kikamilifu.“Jimboni kwangu miundombinu ya maji na afya bado hairidhishi lakini najitahidi kutafuta wahisani pamoja na kushirikiana na serikali ili kuhakikisha kuwa wanaziboresha na kuzisogeza huduma karibu na wananchi,” alisema Chegeni.
“Lakini kikubwa ni serikali kuelekeza huduma muhimu ambazo zitarahisisha maisha.”
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment