Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 24, 2015

Majaliwa: Serikali itatekeleza ahadi zote

Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim
By Mwanja Ibadi, Mwananchi
Ruangwa. Serikali ya Awamu ya Tano imesema itatekeleza ahadi zote zilizotolewa kwa wananchi wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu na kwamba watafanya hivyo kwa kutumia fedha zinazoendelea kukusanywa kwa kutumbua majipu na vyanzo vingine vya mapato.
Waliotoa ahadi wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu kadri ilivyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), walikuwa mgombea urais aliyeibuka mshindi, Dk John Magufuli, na mgombea mwenza ambaye sasa ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya ahadi walizotoa kila walikopita mikoani ni Serikali kutoa elimu bure hadi kidato cha IV, kila kijiji kupatiwa Sh50 milioni kwa ajili ya wajasiriamali, kuboresha huduma za kijamiii kama afya, maji, umeme na ujenzi wa barabara na vyote vinahitaji fedha za kutosha. Ahadi nyingine zilikuwa kurejesha mashamba, na viwanda vilivyobinafsishwa kwa watu lakini vimetelekezwa na kuanzisha mahakama ya mafisadi
Akizungumza jana na wananchi wa kata za Mandawa, Namichiga na Mbekenyera wilayani Ruangwa mkoani Lindi wakati wa ziara ya siku tatu ya kuwashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kumchagua kuwa mbunge wao, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim alisema ahadi hizo zitatekelezeka kwa vile wamejipanga vyema.
Majaliwa alisema Serikali imejipangia kuongeza mapato ya Serikali kwa kukusanya kodi ya Sh1 trilioni kwa mwezi kutoka vyanzo mbalimbali ikiwamo kuwabana wafanyabiashara wakubwa wanaokwepa kodi kwa kuwa fedha za maendeleo ziko huko.
Alisema kodi hizo zinapatikana kwa wafanyabiasha wakubwa ambao kwa muda mrefu wamekuwa hawalipi hali ambayo Serikali ya Awamu ya Tano haiwezi kuivumilia wala kuifumbia macho.
Alisema hawako tayari kuona baadhi ya Watanzania wakinufaika na raslimali za nchi kwani hilo ni jambo ambalo linaweza kuleta mgongano kati ya viongozi na baadhi ya wafanyabisha wasio wazalendo.
Kuhusu huduma za afya, Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka Watanzania kujiunga kwa wingi na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIC) kwani Serikali itaboresha na kuimarisha mfuko huo kwa kudhibiti fedha za wachangiaji ili zitumike kwa ajili ya kupata matibabu bora.
Aidha, aliwaomba wananchi wilayani humo kuwaombea kwa Mungu viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kutokana na kazi ngumu na ya hatari wanayoifanya ya kutumbua majipu bila gazi.     

No comments :

Post a Comment