
Chiku Gallawa.
Musoma. Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Zelothe Stephen ameamuru kutiwa mbaroni Ofisa Afya wa Kata ya Mkendo, Desideri Rwegoshora kwa kushindwa kusimamia usafi katika maeneo ya kata yake.
Zelothe alitoa amri hiyo baada ya kufanya ukaguzi katika kata zote na kubaini mazingira ya kata hiyo yamekithiri kwa uchafu na kukaidi maagizo aliyotoa katika kamati ya usafi ya wilaya.
Alisema katika kata hiyo kuna soko kuu la wilaya linalotegemewa na wakazi wengi wa Musoma, lakini limekithiri kwa uchafu.
Dodoma
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa akizungumza wakati wa kufanya usafi katika soko la Chang’ombe, amepiga marufuku uuzaji wa mifuko ya rambo na kuwaagiza watendaji kukagua mifuko hiyo katika maduka.
Handeni
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Husna Msangi amewataka wafanyabiashara wa kwenye masoko na migahawani kuzingatia kanuni za usafi na kuacha tabia ya kulalamika kuwa Serikali inawanyanyasa.
No comments :
Post a Comment