AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 10, 2015

WAKUU WA MIKOA WAGUFULIKA!

 Wakuu wa mikoa wacharuka, faini ya Sh50,000
By Waandishi Wetu, Mwananchi
Mikoani. Mikoa mbalimbali nchini imeazimia kuwatoza  faini watu wote watu watakaobainika wakitupa taka ovyo ili kupambana na uchafuzi wa mazingira.
Baadhi ya mikoa hiyo, wa Njombe,  umeazimia kufanya usafi katika Hospitali ya Kibena, huku Halmashauri ya Mji wa Njombe ikisema itatumia kila siku ya  Jumamosi kufanya usafi.
Hayo yalisemwa jana na Katibu Tawala wa Mkoa Njombe, Jackson Saitabahu katika maadhimisho ya Uhuru baada ya kufanya usafi kwenye maeneo ya Stendi Kuu ya Mabasi Njombe, Soko Kuu na Hospitali ya Kibena akisema hilo ni agizo kwa watendaji wa Serikali.
Diwani wa Kata ya Njombe, Aggrey Mtambo alisema wamekubaliana katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kuwa kila Jumamosi itakuwa siku ya kufanya usafi wakishirikiana na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Njombe mjini.
Aliwataka wananchi kuacha kutupa taka ovyo ili kutoangukia katika faini ya Sh50,000 na ili kutekeleza hilo wataweka vifaa vya taka kwenye maeneo mbalimbali.
“Kila mwananchi awe mlinzi wa mwenzake na kama atamkamata mtu anachafua mazingira na kumpeleka Baraza la Kata katika ile faini ya Sh50,000, yeye atapata Sh20, 000,” alisema Mtambo.
Mwanza, Ruvuna na Kilimanjaro
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo aliagiza kila Jumamosi iwe siku maalumu ya kufanya usafi jijini humo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu aliuagiza uongozi wa manispaa hiyo kuwakamata na kuwatoza faini ya Sh50,000 watu wanaochafua mazingira kwa makusudi, ili kukomesha vitendo vya uchafu ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani watakaoshindwa kulipa faini.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala aliagiza kufanyika kwa tathmini ya wafanyabiashara ambao hawakujitokeza kufanya usafi ili wachukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka agizo la Rais John Magufuli.

No comments :

Post a Comment