Dodoma. Zilikuwa siku nne ngumu kwa Serikali bungeni. Ndivyo unavyoweza kuelezea hali ilivyokuwa kwenye chombo hicho cha kutunga sheria katika siku za mwanzo za mkutano wa pili wa Bunge la Kumi na Moja.
Mkutano huo ulioanza Jumanne, ulikumbwa na mlolongo wa maombi ya mwongozo kuhusu uamuzi wa kituo cha televisheni cha Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kupunguza matangazo ya moja kwa moja ya shughuli za Bunge.
Jumanne ilikuwa siku ya kujadili hotuba ya Rais John Magufuli, na siku ya pili tu wabunge wa upinzani walihoji uamuzi wa TBC kupunguza matangazo ya moja kwa moja, wakiwasema unawanyima wananchi haki ya kikatiba ya kupata habari.
Jumatano mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko aliuliza swali kuhusu elimu bure na baada ya majibu, wabunge wengi walisimama kutaka kuomba mwongozo na waliponyimwa walipiga kelele zilizosababisha mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kuita polisi ili wawaondoe wabunge wa upinzani kwa nguvu.










Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu Serikali ilivyojipanga kuboresha na kuhudumia sekta mbalimbali nchini ikiwemo elimu, umeme, maji na miundombinu. Kulia ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alfayo Kidata na kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu.










.jpg)