Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, March 26, 2017

Nape Nnauye aibukia Taifa leo, akutana na Dr. Mwakyembe!



Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki waliojitokeza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.

Mashabiki hao walijitokeza kwenda kuishuhudia Taifa Stars ikipambana na Botswana katika mechi ya kirafiki ambayo walishinda kwa mabao 2-0.

Nape naye aliingia kushuhudia mechi hiyo na mashabiki walimshangilia kwa nguvu wakiimba "Nape, Nape, Nape".

Pamoja na kumshangilia, wengi walikuwa wakigongana kutaka kupiga naye picha naye aliwapa nafasi mashabiki hao.

Baadaye, Nape aliungana na Dk Harrison Mwakyembe ambaye amechukua nafasi yake baada ya kuteuliwa na Rais John Pombe Magufuli.

Nape na Dk Mwakywembe walikaa pamoja na kushuhudia mechi hiyo hadi mwisho.

No comments :

Post a Comment