Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, March 26, 2017

Tataki yalaani wasomi wanaokwamisha matumizi ya Kiswahili!

Dar es Salaam. Taasisi ya Taaluma za kiswahili (Tataki) imelaani vitendo vya wasomi, Profesa, na wataalamu mbalimbali wanaopinga matumizi ya lugha kiswahili katika nyanja mbalimbali ikiwamo kutumika kama lugha ya kufundishia.

Hayo yamesemwa leo (jumamosi), na Mkurugenzi wa Tataki, Ernesta Mosha wakati wa maonyesho ya wiki ya utafiti wa lugha ya kiswahili katika miradi mbalimbali iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa lengo la kukuza kiswahili.

Miradi hiyo ikiwamo ya kufundisha lugha ya kiswahili kwa wageni wanaoingia nchini kwa ajili ya kuwapatia Taaluma na namna ya kuwasiliana kwa kutumia lugha ya kiswahili.
Mosha alisema katika wiki hiyo ya utafiti iliyobeba kauli mbiu ya "utafiti wa uchumi wa viwanda na maendeleo ya kati " imelenga kuhamasisha wawekezaji kutoka nje kutumia lugha ya Kiswahili katika mawasiliano.

"Hakuna maendeleo ya viwanda kama hakuna mawasiliano wakati wa uzalishaji hivyo ni muhimu kutumia kiswahili ambacho ndio lugha inayoeleweka nchini" alisema.


No comments :

Post a Comment