Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 26, 2019

Ethiopia yatarajia kuwa kitovu cha biashara ya mtandaoni Afrika!

Nchi ya Ethiopia inatarajia kuwa kitovu muhimu cha biashara ya mtandaoni barani Afrika baada ya kusaini makubaliano ya kuanzisha kituo cha biashara ya mtandao ya Kimataifa eWTP na kampuni ya Alibaba ya China.

Kituo hicho kitajengwa katika mji mkuu Addia Ababa na ni cha kwanza cha aina yake barani humo.

Hafla ya kusaini makubaliano hayo imehudhuriwa na waziri mkuu wa Ethiopia Aby Ahmed, mwanzilishi wa kampuni ya Alibaba Jack Ma miongoni mwa maafisa wengine wa ngazi ya juu kutoka pande zote mbili.
Kulingana na makubaliano hayo, kituo hicho cha eWTP kinakusudiwa kuwezesha biashara baina ya nchi mbalimbali na kutoa mafunzo kwa wajasiriamali hasa vijana.

Jack Ma, akihutubia washiriki wa uzinduzi huo anasema sasa ni wakati wa Afrika wa kujinufaisha na utandawazi kupitia biashara ya mtandaoni.

No comments :

Post a Comment