Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Fredrick Sumaye amesema kwa sasa hawezi kusema chochote kufuatia Kamati Kuu ya CHADEMA kupitisha jina lake peke yake kuwania Uenyekiti Kanda ya Pwani, bali atazungumza mara baada ya kukamilika kwa Uchaguzi wa Kanda hiyo hiyo.
Sumaye ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu ametoa kauli hiyo leo akizungumza na EATV ambapo
amesema bado ni mapema kuzungumzia hilo.
"Kwa sasa siwezi kuwaambia chochote nitaenda kuwaambia hukohuko ndani, ila nikishapita naombeni mnitafute ndiyo nije, lakini kwa sasa siwezi kusema chochote kwa sababu nikifanya hivyo nitakuwa nimefanya tambo za kampeni ambazo mimi sitaki kufanya" amesema Sumaye.
Ikumbukwe uchaguzi wa kanda kwa chama hicho unatarajiwa kufanyika Alhamis ya wiki hii ambapo wagombea mbalimbali majina yao yamepitishwa na Kamati Kuu ya CHADEMA ili kuwania nafasi hizo.

No comments :
Post a Comment