Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 26, 2019

Kikao cha baraza la wawakilishi Zanzibara kuanza !


Jumla ya Maswali 96 yameratibiwa kuulizwa na kujibiwa katika Mkutano wa 16 wa Baraza la Tisa la Wawailishi Zanzibar ambao unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano Novemba 27 mwaka huu saa tatu kamili Asubuhi.

 Akitoa Taarifa kwa vyombo vya habari, Katibu wa Baraza hilo Raya Issa Msellem alisema katika Mkutano huo jumla ya maswali 96 yataulizwa na kujibiwa na wajumbe wa baraza hilo.

Alisema mbali na maswali na majibu katika mkutano huo kutawasilishwa kwa miswaada mbali mbali ya sheria ambayo iliwasilishwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa Septemba mwaka huu.
 “Miswada hiyo sasa itasomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa katika mkutano huu wa 16” Alisema Katibu huyo.

Alieleza Miswada yenyewe ni Mswada wa Sheria ya kuanzisha wakala wa Serikali mtandao, kazi zake na mambo mengine yanahusiana nayo.

Pia Mswada wa Sheria ya  Marekebisho ya Sheria ya kuanzisha Ofisi ya Mufti, Namba 9 ya mwaka 2001.

 “Mswada mwingine ni Mswada wa Sheria ya marekebisho ya sheria mbali mbali nakuweka masharti bora ndani yake” alieleza katibu huyo wa Baraza la Wawakilishi.

 Aliongeza kwa kueleza kuwa Mswada mwingine ni mswada wa Sheria ya marekebisho ya Sheria ya usafiri barabarani ya Namba 7 ya mwaka 2003 pamoja na Mswada wa Sheria ya kuanzisha wakala wa barabara Zanzibar na mambo mengine yanayohusiana nahayo.

 Katika maelezo yake katibu Raya alisema kuwa katika Mkutano huo wajumbe wanatarajia kupokea mswada kwa hati ya dharura ya kuanzisha Sheria ya kuanzisha kwa chuo cha mafunzo ya Sheria kwa vitendo (law School).

No comments :

Post a Comment