
Hii ni baada ya kamishna wa shirika hilo lenye wanachama 55 barani Afrika, Moussa Faki Mahamat na mafisa wengine wa ngazi za juu katika AU, kukamilisha ziara ya siku mbili nchini Afrika Kusini huku wakifanya mazungumzo na Rais Ramaphosa pamoja na maafisa wa serikali nchini humo.
Taarifa kutoka shirika la AU lilisema kuwa viongozi hao wawili walijadili mikakati na maswala ambayo Afrika Kusini itazingatia itakapochukua usukani kama mwenyekiti wa AU, huku Ramaphosa akisisitiza umuhimu wa kupatikana kwa suluhu na amani katika nchi ya Libya.
No comments :
Post a Comment