Rais John Magufuli amekubali kuanza kulipa deni la nyumba zaidi ya 6000 zilizojengwa nchini kwaajili ya makazi ya askari wa JWTZ lililoiva na kufikia zaidi ya trilioni Moja.
Ameyasema hayo leo wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja wa maadhimisho ya kitaifa Ikulu Chamwino, aweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) katika eneo la Kikombo.
"Kwa mkataba tuliosaini sisi wenyewe serikali kwa wakati ule tulisaini kwamba nyumba hizi zikijengwa wanajeshi watakuwa wanakatwa kwa watakaokuwa wanakaa humo. Tumeshazungumza na waziri, na leo CDF amezungumza hapa, huwezi ukamchukua askari ambaye nyumba anayokaa kwenye maeneo ya kiaskari halafu unaanza kumtoza fedha..
Ameendelea kwa kusema, "Ninafahamu deni hilo ni fedha nyingi, ninahakikishia hakuna kukatwa askari yeyote hilo deni litabebwa na serikali. Nafikiri kesho ama kesho kutwa wataanza kulilipia hilo deni ambalo limeivaa, wataanza kwa kulipa dola zaidi ya milioni 25 akini siwezi kuwaweka maaskari wangu kwenye utumwa wa kulala.
Pia Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa jengo la Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB) na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji Jijini Dodoma.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

No comments :
Post a Comment