
Katika rufaa hiyo, Nondo anawakilishwa na Mawakili watatu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania ambao ni Wakili Jebra Kambole, Chance Luoga na Shilinde Swedy.
Itakumbukwa kwamba Nondo alishtakiwa mwaka 2018 mwezi Machi kwa kutoa taarifa za uongo kinyume na Kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa Mtandaoni, ya mwaka 2015.
Hata hivyo, mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa ilitoa maamuzi na kumpa ushindi Nondo kwa kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha mashtaka yao pasipo shaka. Baada ya kushindwa katika mahakama hiyo, upande wa Jamhuri walikata rufaa mahakama kuu kanda ya Iringa na usikilizwaji wa rufaa hiyo umepangwa kesho mbele ya Mhe. Jaji Penterine Kente.
No comments :
Post a Comment