dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, August 23, 2012

COMPARE THE 2 BAADAE MEZEA!!!


Wa kwetu akitembelea miradi yake huko Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani!


Wa wenzetu akiwajengea watu wake makaazi bora nje kidogo ya Kigali!

Wakubwa wachague either kuendeleza miradi yao binafsi au kuwatumikia wananchi!
Rushwa bado nchini ni adui mkubwa kwa wananchi!

Na Geo Kimbi
August 23, 2012

Zanzibar, Tanzania.
Hapo juu tunamuona Rais Kikwete na mama Salma Kikwete pamoja na mjukuu wao shambani kwao. Kwa kweli inafurahisha sana picha kama hio. Zaidi, Rais Kikwete ni mkulima na mfugaji na yupo siku zote mbele katika kuendeleza na kutekeleza sera ya Serikali ya kusukuma kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya sekta ya kilimo nchini. Kwa hilo tunampa hongera na tunampigia makofi. Kwa upande mwengine tunasikitika sana sana sana!

Tunasikitika sana kwasababu japokuwa kilimo ndio hobby yake Rais Kikwete lakini shamba lake la kijijini Msoga ambalo lipo nje kidogo ya Chalinze, Mkoa wa Pwani ni zaidi ya hobby. Huu ni mradi wake na kwa Rais wa nchi (wachilia mbali mawaziri na wakubwa wengine) kuwa mwenye miradi binafsi ni makosa, kwasababu anakuwa easily susceptible to corruption na corruption leo katika Tanzania ndio adui wetu mkubwa.
Kwani shida yetu sisi Watanzania inasababishwa na nini? Kujibu hili suala labda nimnukuu Mtanzania mmoja aitwae Said Sudi ambae aliwahi kuandika huko nyuma kuwa...” Problem yetu sisi ni kuwa kila mmoja wetu yupo busy na biashara zake za pembeni na kazi za serikalini tunazipa lipservices tu!
Inaumiza kuona vipi mtu anakuwa serikalini na bado anaruhusiwa kuwa na miradi mikubwa mikubwa ya kwake pembeni, …….
Either uwatumikie wananchi au jitumikie mwenyewe, lakini huwezi kuwa huku na huku! Hii ndio inayoturudisha nyuma siku zote”. Ninaongezea hapo kuwa na kama wakubwa wakiwa na miradi yao pembeni under the guise of hobbies basi vita ya kupambana na rushwa na kustawisha utawala bora nchini itakuwa ni ndoto.
Hatusemi kuwa Rais Kikwete aacahe hobby yake ya ukulima, lakini Rais ni Project Manager wa projects zote nchini na halafu yeye kuwa anayo project nyengine ya kwake pembeni ya kui-manage hatujui namna atakavyozi-manage projects zote hizo za nchi kwa pamoja. Hata kama ataweka ma-managers tele ku-manage kazi zake binafsi hizo za ukulima huko shambani kwake, his input will always be needed and this will be at the expense ya muda wa kuwahudumia wananchi na nchi!
Tusije tukasahau kuwa uwaziri au uraisi ni kazi ya masaa 24/7 na sio kazi ya 8-hours or 12-hours shift!
Hatuwezi kuupiga vita umaskini nchini kwetu kama nguvu zetu zote hazimlengi adui huyo. Hulka hii ya wakubwa zetu ya kuwa kila mmoja anamiradi yake pembeni itatufanya wengi wetu tuendelea kuzama kwenye lindi la umaskini japokuwa nchi yetu ni yenye utajiri mkubwa wa madini na ardhi nzuri!

Source: Wagagagigikoko News Network (Wanene)

No comments :

Post a Comment