Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, August 21, 2012

KIKWETE AMKATA MAINI 
MOBHARE MATINYI PIA!
Bw. Matinyi kazizowea siasa za kikoloni
Hata Unguja atataka ivamiwe ikitaka kuacha Muungano

Na Geo Kimbi
August 21, 2012


Above: Mr Mobhare Matinyi who is still living under the delirium of colonization!

Zanzibar, Tanzania.
Kwa RAIS Jakaya Kikwete kusema kuwa hajaliagiza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupigana vita na Malawi kwa sababu za mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya nchi hizo mbili aliwakata maini sio Membe na Lowassa tu, bali mpaka yule muandishi mkorofi wa gazeti la The Citizen anaejulikana kwa jina la mapambano (nom de guerre) kama Mr Eagle, wakati jina lake hasa ni Mobhare Matinyi.
Katika ukumbi wa Wanabidii Bw. Matinyi bila ya haya na bila ya kuwa amelewa gongo alinukuliwa akiandika…" …invade Malawi (because Lilongwe won't listen), kick out every stupid guy and restore a new sensible government. We did it in Uganda, why not in Malawi? After all Joyce Banda has already said that she is ready to die for her country - so let us help her."
"Huyu Bw. Matinyi amezowea. Huko nyuma keshasema madudu tele kuliko haya. Zaidi, alipiga vifirimbi na vigelegele kule kwenye ukumbi wa Wanabidii pale alipouliwa Ghadafi. Uzalendo wa Bw. Matinyi pia unatia shaka sana, kwasababu kwanza hampendi Maalim Seif na pili hataki Unguja iwe huru na anauunga mkono Muungano kuliko Abeid Karume au Julius Nyerere", alieleza muandishi mmoja wa Wagagagigikoko ambae aliwahi kunywa nae maji ya dhahabu kwenye klabu moja kule Washington, DC.
"Tizama hata yule rafiki yake kutoka Kenya aitwae Richard Mgamba hakufurahia  maneno hayo ya Bw. Matinyi na alimsulubu rafiki yake kipenzi huyo kwa kuandika…." But again in this 21st century, it's really appalling for an intellectual like you (Matinyi) to advocate invasion of a foreign country as well as imposing the leadership of your choice. These were the brutal ideas of George Bush, Condoleeza Rice, Dick Cheney and Donald Rumsfeld—but they failed in Iraq as well as Afghanistan." Aliendelea ndugu huyo huku akiangusha kicheko kikubwa cha masikitiko.
But, nothing is appalling to Mr Matinyi who has always been advocating openly for  invasion of other countries, like Libya, Syria, Iran etc. Mr Matinyi who still seems to be living in a delirium of colonization will definitely be the first one to advocate the invasion of Zanzibar once Zanzibaris decide to steer away from the Mainland's  brutal rule.

Source: Wagagagigikoko News Network


5 comments :

  1. Kwanza, jina la safu si jina la mwandishi. Mimi ni Mobhare Matinyi na safu inaitwa kwa kutumia jina la ndege tai ambaye sifa yake ni kuwa na macho makali. Hii ni kawaida ya majina ya safu. Safu yangu huitwa With an Eagle's Eye, na hakuna uthibithso kwa msomaji yeyote kwamba ni mimi niliyekuja na jina hili. Mimi sina jina la uandishi wala la utani, bali hutumia jina langu kamili.
    Pili, nilichokieleza kinapaswa kuangaliwa katika muktadha wake, kwamba, iwapo Tanzania itanyimwa haki yake, na kuthibitika kwa njia zote kwamba imeporwa sehemu ya ziwa, basi italazimika kupigana na hili ni jambo linaloungwa mkono na sheria za kimataifa. Ukipigana vita ni lazima umalize kazi kwa kuung'oa madarakani utawala ulioileta vita hiyo - - tangu enzi na enzi ndivyo ilivyo. Kutoa tamko la maana hii haina maana kwamba mtoa tamko anataka vita sasa bali anaikubali vita kama njia ya lazima lakini ya mwisho.
    Tatu, suala la Zanzibar halifanani na la Malawi isipokuwa kwa mtu asiyejua anajadili nini. Lakini pia sikusema kitu kuhusu Zanzibar ama Muungano.
    Nne, alichokisema Rais Kikwete hakiondoi uwezekano wa Tanzania kuingia vitani. Amesema: "Tuiachie diplomasia ifanye kazi." Kwa mtu mwenye ufahamu maana yake ni kwamba Tanzania inataka utatuzi kupitia njia za kidiplomasia na lazima uwe kwa manufaa yake. Iwapo Malawi itakataa katu kata, unafikiri Kikwete atasema basi tumeshindwa? Hapana! Itafuata njia nyingine kama ya kusaka msuluhishi na baadaye mahakama. Baada ya hapo je?
    MUHIMU: Siasa za kimataifa zinahitaji uelewa mpana wa mambo na si suala la yeyote kutoa wazo lolote. Haya si masuala ya kila mtu kujisema tu, kama ndugu yangu ambaye ameshindwa kuelewa nilichosema na pia ameshindwa kupata ulinganifu sahihi. Inahitaji kupekua makarabrasha kwanza ili kufahamu matamko ya marais wakati wa hali kama hivi huwa yakoje, sababu za nchi kuingia vitani, migogoro ya mipaka ilivyo, sheria za kimataifa, na sera ya Tanzania na hata historia pia, achilia mbali siasa.
    Asante,
    Mobhare Matinyi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Matinyi, umeongea sana lakini naona hujakanusha hiyo war mongering rhetoric juu ya malawi " …invade Malawi (because Lilongwe won't listen), kick out every stupid guy and restore a new sensible government. We did it in Uganda, why not in Malawi? After all Joyce Banda has already said that she is ready to die for her country - so let us help her."

      Katika maandishi yako hayo umeonekana kuwa mzembe wa kutumia hekima na mchochezi wa amani. Ni sad story for self branded intelectual anayefikiri na kuzungumza kwa kinywa cha namna hii. Ni unfortunate kwa Tanzania kuwa na watu waliokosa insaf ya ubinaadamu na wenye kuglorify maamuzi ya kutumia nguvu katika masuala madogo miongoni mwa fellow brothers and sisters of Africa. Shame on you.
      Foum.

      Delete
  2. Nd. Matinyi na Nd. Foum,
    Tunashukuru kwa michango yenu. Kustahamiliana ni wajibu.
    Nasi tutafika tu. At least tunafurahi kuwa katika Tanzania yetu ya leo tunaweza kujieleza bila ya kuogopa kuingiliwa na wakubwa au na vyombo vya Dola. Let's keep it up!
    Admin

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jamani, technology imeleta mengi. wengi wanachangia kwa mtizamo tofauti kwa sababu wana upeo tofauti. Tuvumiliane na tusionyeshe chuki ambazo hazijengi. Matinyi, ni mwandishi msomi sio tu ya uandishi wa habari, bali ana ufahamu wa mambo mengi ya siasa za kimataifa. Ametoa maono yake ambayo mimi binafsi naona yana element ya "critical thinking" . Sisi tunashukuru kwamba tuna wasomi kama kina matinyi ambao wanaabudu freedom of speech na wanatumia usomi wao kuisadia jamii. Big up my brother matinyi, keep it up

      Delete
  3. Throughout history, diplomacy has never been the only solution to all the problems countries face in relations with other countries. Had that been the case, there would have been no need for countries to have armies. As Carl von Clausewitz said, war is the continuation of politics by other means.

    Matinyi is right when he says a military solution to the dispute between Tanzania and Malawi over Lake Nyasa is a viable option to resolve the conflict. And it is true Joyce Banda said she was ready to die for what she considered to be her country's right to exclusive ownership of the contested part of Lake Nyasa; so should we. And that means war.

    Thank you Matinyi for your bold defence of our rights. I have always been impressed by your brilliant analyses of a wide range of issues. I also believe that detractors will never discourage you from doing what you are doing. Keep up the good work.

    Best wishes.

    ReplyDelete