Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, August 21, 2012

Kutoka mablog ya Wazanzibari!
KUH: JENGO JIPYA LA AIRPORT YA ZANZIBAR:
Wazanzibari wasema kwenye tovuti lao la Mzalendo.net kuwa:
Meneja wa Ufundi wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Zanzibar ajiuzulu
Meneja hajuwi kinachoendelea wala hajuwi hilo jengo limejengwa kwa madhumuni gani.

Na Said Bakar
August 21, 2012.

Zanzibar, Tanzania.
Kabla hata sherehe adhimu zinazoendelea Visiwani za kumalizika kwa  mwezi mtukufu wa Ramadhani hazijamalizika, Wazanzibari kwa mara nyengine tena wanachacharika kwa kusema kuwa Menejea wa Ufundi wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Zanzibar Bw Mzee Abdalla Mzee ajiuzulu mara moja, kwani hajuwi kinachoendelea wala hajuwi hilo jengo jipya la Airport ya Zanzibar linalojengwa ni kwa madhumuni gani.
ZANZIBAR | Abeid Amani Karume International Airport Terminal II Extension

Kabsha hizi zimekujaa pale Bw. Mzee alipozungumza juzi tarehe 18 Augusti na vyombo mbalimbali vya habari vilivyofika katika kiwanja cha kimataifa cha ndege Zanzibar, kwa ajili ya kupata maelezo juu ya ujenzi wa kiwanja hicho. Alivyoulizwa vipi hicho kiwanja kitatumika Bw. Mzee alijibu kuwa... “Tutaangalia uwezekano kama tutumie kwa wageni pekee na wenyeji watumie ule wa awali au laa”.
Majibu hayo yaliwakasirisha sana na kuwanyima raha Wazanzibari wakati huu wa sherehe za Eid kule kwenye tovuti lao la  Mzalendo.net na kumtaka Bw. Mzee ajiuzulu wadhifa wake mara moja, kwasababu waliona kuwa hafai.
Mzanzibari mmoja mwenye jina la mapambano (nom de guerre) la Ashakh na kwenye mabano akijiita Kiongozi – yaani Kiongozi wa Mapambano alilalamika na kuandika........” Hivi jamani tumesoma nini ikiwa vijambo kama hivi vidogo akilini mwetu havimo. Sikusudii kukebehi wala kujejea lakini kama ni mimi Meneja wa Ufundi tayari nimeshajuwa najenga jengo jengine kwa madhumuni gani.”
“Hapa inaonekana huyu meneja hajuwi kinachoendelea wala hajuwi hilo jengo limejengwa kwa madhumuni gani. Ikiwa anajuwa, mambo haya angeweza kuyaweka wazi:
- Jengo jipya limetumia mkopo wa USD 70.4 milioni, vipi mkopo huu utalipwa na kwa muda gani. Hivyo tutakuwa tunahitaji abiria wangapi kila mwaka ili waweze kucompensate hii gharama.
- Ikiwa huu ni internationala airport jee kunahaja ya kuendelea kutumia jengo la zamani au abiria wote wafaidi zile facilities za international, hivyo kuongeza mapato
- Mipango yao ikiwa mpaka leo haijulikani, hivyo wanatumia dira gani kufikia lengo lao.”
Aliendelea Nd. Kiongozi na kuandika kuwa...”Tunauhaba wa skills hata kwa wale ndugu zetu walionayo madigree, ma master, na maphd iwe wamesoma ndani au nje ya nchi” Alimalizia Kiongozi.
Mzanzibari mwengine ambae inaonesha tayari keshachukuliwa na swaumu ya kufunga sita aliandika...” Upuuzi mtupu kwa nini wageni wasitumie wazamani, Sisi watu weusi tukiwa Ulaya tunabaguliwa tukiwa hapo Ethiopia tu tunafanywa kama ma.. ya paka,.....Pumbavvv. Alikemea Bw/Bi Nuramo.
Yule mgabachori aitwae Said Sudi yeye aliwafananisha Wazanzibari kuwa ni sawa na vichwa vya wendawazimu. “Hii airport imeliwa sana na wakubwa na itakuwa upuuzi mtupu. Corruption katika wizara ya Mawasiliano inanuka. Airport moja kujenga - Mikataba miwili, uliona wapi?. Kila mmoja akitaka Mkataba wake ndio utiwe sahihi na Contractor” Aliendelea kijana mwengine nje ya hili tovuti.
Kwani ni nini hasa shida yetu sisi Wazanzibari? Ndugu Said Sudi anajibu suala hilo pale alipoandika kuwa...” Problem yetu sisi ni kuwa kila mmoja wetu yupo busy na biashara zake za pembeni na mambo ya kazini tunayapa lipservices tu!
Inaumiza kuona vipi mtu anakuwa serikalini na bado anaruhusiwa kuwa na miradi mikubwa mikubwa ya kwake pembeni, kama mahoteli, etc etc?
Either uwatumikie wananchi au jitumikie mwenyewe, lakini huwezi kuwa huku na huku! Hii ndio inayoturudisha nyuma siku zote”.
Bw. Mzee aliliwazwa kidogo pale Nd. Sweethome alipoaandika kutoka Denmark kuwa...."jamani punguzeni jazba kidogo mimi nilivyofahamu ni kama hivi:
jenge jipya linauwezo wa kuchukua abiria 800 kwa wakati mmoja, tukumbuke kwamba watu hawakai airport siku nzima.
ukuchukua makdirio yao ya watu 1,100000 kwa mwaka. ukigawa na siku 360 za mwaka (makadirio)
utapata kiasi cha watu 4000 kwa siku, logically hii inakubalika, ni karibu na watu 150 kwa saa.
sasa ukilinganisha na kimoja kati ya viwanja vikubwa kabisa dunia let take cph(copenhagen ) airport, inachukua abia million 22 kwa mwaka. ukigawa na siku 360..kwa wastani wanaingia watu 60,000 kwa siku, na ni wastani wa watu 2500 kwa saa.
ukitizama hizo tal, utaona kwamba, kwa ukubwa wa znz na population yake.kiwanja kitakidhi haja bila ya wasi wasi wowote.
na kuhusu matumizi ya jengo, hapa kuna tricky kidogo. tufahamu kwamba viwanja vingi vikubwa duniani vimegawika sehemu mbili au tatu kwa europe, sehemu ya international, ya euro na ya local passangers. kwa kurahisisha process na kufanya uwanja uwe effectiv.
lakini matumaini yangu hiyo sehemu itakayo tumiwa na ndege za local i we na hadhi nzuri,
nawasilisha", alimalizia.
Lakini mpiganaji Kiongozi Nd. Ashakh hakukubali maneno hayo ya Nd. Sweethome kutoka Denmark na wala jazba hakupunguza na akaendelea kumvurumishia Bw. Mzee makombora na akaandika kuwa…."Hoja yetu kubwa ni kwa hii mipango ya awali, ikiwa mpaka sasa menega ufundi hujuwi uwanja mpya utakuwa wa wageni au laa. Wenyeji wao huenda wakapelekwa uwanja mkongwe. Swala linakuja hivyo tulipokuja na hili shauri la kujenga uwanja mpya tulikuwa hatuna mipango ni kwa ajili ya nani?", aliulizwa Nd. Sweethome.
Nd. Ashakh akiona kwamba hakuna njia ya kumuokoa Mzanzibari kutokana na sabotage anayoipata kutoka kila upande, alimalizia maneno yake na huku bila ya shaka akitokwa na machozi na kusema…." Kuku wa masikini hatagi, hata akitaga halalii, na akilalia haangui, akiangua halei."

Na Said Bakar wa Wagagagigikoko News Network




No comments :

Post a Comment