MWAKA 2001 Uingereza iliingiza kwenye sensa swali la Dini. Walifanya hivyo baada ya kufanya utafiti na kusikiliza wananchi wanataka nini, ninamnukuu mwandishi Aspinall anasema "The decision to include the question was made subject to general public support, as assessed in the June 1997 Census Test (97,000 households in Great Britain), the April 1999 Rehearsal (114,800 households in England and Wales), and other public consultation exercises." (Aspinall, 2000).
TARJUMA: Uamuzi wa kuliingiza swali umefanyika baada ya jamii kuliunga mkono, kama ilivyotafitiwa mwezi Juni 1997 katika sensa ya majaribio [Nyumba 97,000 za Great Britain], na zoezi la mwezi April 1999 (Hyumba 114,800 za England na Wales) na mazoezi mengine yaliyofanyika kwenye umma.
Cha kusikitisha sana ni kuwa serikali ya Tanzania inapuuzia wito wa kundi fulani la wananchi juu ya suala sawa na hili. Tena Tanzania tunaambiwa haina Dini, hivyo kimtazamo hili lilikuwa liwe jambo rahisi. Uingereza ni nchi ya Kianglikana, hivyo wangeweza kusema kwamba nchi hii inaendeshwa kianglikana kwa hiyo suala la dini halina maana yoyote, lakini hawakufanya hivyo.
Baadhi ya nukta muhimu za kuzingatia kuhusu kuingiza suala la dini katika sensa.
::::: LESENI ZA BIASHARA ::::::
Si jambo sahihi kuweka bishara ambayo haiendani na maadili ya jamii au watu wa eneo husika. Moja kati ya kesi maarufu ambayo imewahi kutokea Duniani ni McDonald kuuza nyama ya ng'ombe katika Fast Food za India. Hili lilikuwa ni tusi kwa mabaniani kwani kwao wao Ngo'mbe ni Mungu. McDonald iliomba msamaha na wakaacha mara moja kuuza Beaf Burger (baga za nyama ya ng'ombe) katika maeneo yenye mahindu wengi nchini India. Tafadhali kumbuka kadhia ya mabucha ya nguruwe Dar -es -salaam katika maeneo ya waislamu wengi katika miaka ya tisiini.
Hivyo hii itasaidia serikali kujua ni wapi pakutoa aina fulani ya leseni ya biashara kulingana na dini ya watu wa eneo hilo.
::::::::: NYUMBA ZA IBADA ::::::::
Ni imani yangu kuwa moja kati ya sababu za kuchomwa makanisa huko Zanzibar ni kuwepo kwa makanisa katika maeneo yasiyostahiki (hii inahitaji utafiti zaidi) kwa sababu katika maeneo ambayo makanisa yale yalijengwa ni mitaani na ni mitaa yenye waislamu wengi mno kulinganisha na wakristo wenyewe.
Matokeo yake makanisa yamechomwa moto. Tafadhali mimi siungi mkono kuchomwa moto kwa makanisa yale, kitendo kile kilikuwa ni uvunjaji wa sheria, lakini je kujenga makanisa yale katika maeneo yale ilikuwa sahihi?
Moja kati ya kesi maarufu Duniani ni ile ya Waislamu kukataliwa kujenga msikiti katika kiwanja chao kilichopo karibu na Ground zero (New York) na sababu ya msingi ni kwamba wakaazi wa eneo hilo wengi wao ni wakristo halafu bado wana uchungu wa tukio la Septemba 11, hivyo huenda ingepelekea waisalmu kudhuriwa iwapo serikali ingetoa kibali cha kujengwa msikiti ule. Haya ni maamuzi ya busara ambayo yanaepusha matatizo ya baadae, maamuzi haya yanaweza tu kuchukuliwa iwapo serikali inatambua dini za watu wa eneo husika. Hivyo hii inaonyesha umuhimu wa kuuliza dini za wahusika.
:::::::::::: MISREPRESENTATION (KUTOWAKILISHWA) ::::::::::
Ni utaratibu unaokubalika nchini Tanzania kwamba kila kundi katika umma au jamii linahitaji uwakilishi katika mambo mbali mbali ya kimaendeleo. Bunge la Tanzania hutoa viti maaum vya upendeleo kwa wanawake kwa sababu kuna kutowakilishwa kwa wanawake katika Bunge. Hivyo ni wazi kuwa kila kundi katika jamii lina haki ya kuwakilishwa katika sehemu na ngazi mbali mbali za uongozi na sehemu zinazohusika na maendeleo ya jamii. Ndio maana kunakuwepo na nafasi za upendeleo (positive segregation) ili kuzipa jamii uwakilishi wa haki.
:::::::::::::TENSION ZA UDINI :::::::::::::
Ni wazi kuwa Tanzania inakabailiwa na tatizo la UDINI. Moja kati ya njia ya kuuvunja udini ilikuwa ni kujenga jamii ambayo kila kundi likapewa haki yake na likajihisi linapata haki zake, kujihisi kuwa umepata haki ni jambo la muhimu kwani Tanzania inaamini kwa < > Yaani haki sio tu itendeke bali pia ionekane kuwa imetendeka. Lakini leo serikali ya Tanzania imekuwa ikipuuza masuala ya UDINI na kudhani suluhu ni kufukia madai na kelele za makundi mbali mbali. Kamwe hili sio suluhisho na ule "uongo" Tanzania haina Dini lakini Watanzania wana Dini ni wazi kuwa haufanyi kazi sasa hivi.
Mwisho ningependa kumnukuu tena Aspinall anasema:
"Information on religions will meet government needs arising from the increasing involvement of faith communities as collaborators in urban regeneration and health improvement. (Aspinall, 2000)
Tarjuma:
<> (Aspinall, 200)
Ndio maana leo Nandos na kampuni nyingi kubwa za vyakula nchini Uingereza vinauza vyakula halali katika miji kama vile Leicester na Birmingham, hii inawanufaisha wananyabishara na pia wananchi kwa vile wanafahamu kuwa hii ni miji yenye Waislamu wengi.
Reference:
Aspinall, P 2000, 'Should a Question on 'Religion' be Asked in the 2001 British Census? A Public Policy Case in Favour', Social Policy & Administration, 34, 5, pp. 584-600, Academic Search Premier, EBSCOhost, viewed 23 August 2012.
Appendix:
https://www.census.ac.uk/Documents/CensusForms/2001_England_Household.pdf
Hii ni specimen ya fomu halisi ya Population Census ya UK in 2001, angalia ukurasa wa sita swali namba 10, linauliza "What is your religion?" Hivyo Waislamu kudai kuingizwa swali hili sidhani kama ni kiroja kipya katika Population Census.
www.census.ac.uk
Source: Mapara
No comments :
Post a Comment